Guru Granth Sahib Translation Project

Guru Granth Sahib Swahili Page 474

Page 474

ਪਉੜੀ ॥ pa-orhee. Pauree:
ਆਪੇ ਹੀ ਕਰਣਾ ਕੀਓ ਕਲ ਆਪੇ ਹੀ ਤੈ ਧਾਰੀਐ ॥ aapay hee karnaa kee-o kal aapay hee tai Dhaaree-ai. Ee Mungu, Wewe Mwenyewe umeumba uumbaji, na Wewe Mwenyewe umeweka nguvu Yako ndani yake.
ਦੇਖਹਿ ਕੀਤਾ ਆਪਣਾ ਧਰਿ ਕਚੀ ਪਕੀ ਸਾਰੀਐ ॥ daykheh keetaa aapnaa Dhar kachee pakee saaree-ai. Wewe unatazama uumbaji Wako kama mchezo wa ubao na kuamua ni vipande (binadamu) vipi ni vya kweli (ambao wametimiza kusudi lao la maisha ya kibinadamu) na vipi ni vya uongo.
ਜੋ ਆਇਆ ਸੋ ਚਲਸੀ ਸਭੁ ਕੋਈ ਆਈ ਵਾਰੀਐ ॥ jo aa-i-aa so chalsee sabh ko-ee aa-ee vaaree-ai. Yeyote aliyekuja duniani humu, ataondoka; wote watakuwa na wakati wao.
ਜਿਸ ਕੇ ਜੀਅ ਪਰਾਣ ਹਹਿ ਕਿਉ ਸਾਹਿਬੁ ਮਨਹੁ ਵਿਸਾਰੀਐ ॥ jis kay jee-a paraan heh ki-o saahib manhu visaaree-ai Yeye anayemiliki roho yetu, na pumzi yetu ya uhai – kwa nini tumsahau Bwana Huyo kutoka akilini mwetu?
ਆਪਣ ਹਥੀ ਆਪਣਾ ਆਪੇ ਹੀ ਕਾਜੁ ਸਵਾਰੀਐ ॥੨੦॥ aapan hathee aapnaa aapay hee kaaj savaaree-ai. ||20|| Tunafaa kufanikisha kazi yetu ya kuungana na Mungu wenyewe, kwa kutafakari kuhusu Jina Lake.
ਸਲੋਕੁ ਮਹਲਾ ੨ ॥ salok mehlaa 2. Salok, na Guru wa Pili:
ਏਹ ਕਿਨੇਹੀ ਆਸਕੀ ਦੂਜੈ ਲਗੈ ਜਾਇ ॥ ayh kinayhee aaskee doojai lagai jaa-ay. Huu ni upendo wa aina gani, ambao unakwama kwa uwili (kumpenda mwengine ila Mungu)?
ਨਾਨਕ ਆਸਕੁ ਕਾਂਢੀਐ ਸਦ ਹੀ ਰਹੈ ਸਮਾਇ ॥ naanak aasak kaaNdhee-ai sad hee rahai samaa-ay. Ee Nanak, yeye tu anafikiriwa kuwa mpenzi wa kweli, anayesalia kuzama katika upendo wa mpendwa (Mungu) wake milele.
ਚੰਗੈ ਚੰਗਾ ਕਰਿ ਮੰਨੇ ਮੰਦੈ ਮੰਦਾ ਹੋਇ ॥ changai changa kar mannay mandai mandaa ho-ay. Lakini yule anayefurahia wakati tu vitu vizuri vinatendeka, na kukataa wakati vitu vinatendeka vibaya,
ਆਸਕੁ ਏਹੁ ਨ ਆਖੀਐ ਜਿ ਲੇਖੈ ਵਰਤੈ ਸੋਇ ॥੧॥ aasak ayhu na aakhee-ai je laykhai vartai so-ay. ||1|| Hastahili kuitwa mpendwa wa kweli wa Mungu, kwani yeye anahusiana na Mungu kwa mtindo wa kibishara.
ਮਹਲਾ ੨ ॥ mehlaa 2. Salok, Guru wa Pili:
ਸਲਾਮੁ ਜਬਾਬੁ ਦੋਵੈ ਕਰੇ ਮੁੰਢਹੁ ਘੁਥਾ ਜਾਇ ॥ salaam jabaab dovai karay mundhhu ghuthaa jaa-ay. Yule anayetoa salamu za heshima na kumkataa kwa kiburi Bwana wake, anapotoka kimsingi kutoka mwanzo.
ਨਾਨਕ ਦੋਵੈ ਕੂੜੀਆ ਥਾਇ ਨ ਕਾਈ ਪਾਇ ॥੨॥ naanak dovai koorhee-aa thaa-ay na kaa-ee paa-ay. ||2|| Ee Nanak, tabia hizi mbili sio za kweli, na hazikubaliki katika mahakama ya Mungu.
ਪਉੜੀ ॥ pa-orhee. Pauree:
ਜਿਤੁ ਸੇਵਿਐ ਸੁਖੁ ਪਾਈਐ ਸੋ ਸਾਹਿਬੁ ਸਦਾ ਸਮ੍ਹ੍ਹਾਲੀਐ ॥ jit sayvi-ai sukh paa-ee-ai so saahib sadaa samHaalee-ai. Kumtafakari ambaye kwake amani inapatikana; Bwana huyo daima anafaa kukumbukwa.
ਜਿਤੁ ਕੀਤਾ ਪਾਈਐ ਆਪਣਾ ਸਾ ਘਾਲ ਬੁਰੀ ਕਿਉ ਘਾਲੀਐ ॥ jit keetaa paa-ee-ai aapnaa saa ghaal buree ki-o ghaalee-ai. Tukifahamu kwamba ni sharti tuhimili matokeo ya vitendo vyetu, basi kwa nini tutende vitendo viovu?
ਮੰਦਾ ਮੂਲਿ ਨ ਕੀਚਈ ਦੇ ਲੰਮੀ ਨਦਰਿ ਨਿਹਾਲੀਐ ॥ mandaa mool na keech-ee day lammee nadar nihaalee-ai. Hatufai kufanya uovu wowote hata kidogo; tunafaa kufikiria matokeo yake kwanza.
ਜਿਉ ਸਾਹਿਬ ਨਾਲਿ ਨ ਹਾਰੀਐ ਤੇਵੇਹਾ ਪਾਸਾ ਢਾਲੀਐ ॥ ji-o saahib naal na haaree-ai tavayhaa paasaa dhaalee-ai. Tunafaa kuucheza mchezo wa maisha kwa njia ambayo hatutafikirwa kuwa washindwa mbele ya Bwana wetu.
ਕਿਛੁ ਲਾਹੇ ਉਪਰਿ ਘਾਲੀਐ ॥੨੧॥ kichh laahay upar ghaalee-ai. ||21|| (kwa maisha haya ya kibinadamu yenye thamani), tunafaa kufanya vitendo ambavyo vitatuletea staha katika mahakama ya Mungu.
ਸਲੋਕੁ ਮਹਲਾ ੨ ॥ salok mehlaa 2. Salok, Guru wa Pili:
ਚਾਕਰੁ ਲਗੈ ਚਾਕਰੀ ਨਾਲੇ ਗਾਰਬੁ ਵਾਦੁ ॥ chaakar lagai chaakree naalay gaarab vaad. Iwapo mtumishi atafanya huduma, kwa ubinafsi na mabishano,
ਗਲਾ ਕਰੇ ਘਣੇਰੀਆ ਖਸਮ ਨ ਪਾਏ ਸਾਦੁ ॥ galaa karay ghanayree-aa khasam na paa-ay saad. Yeye anaweza kuzungumza kiasi anachotaka, lakini hatakuwa wa kupendeza kwa Bwana wake.
ਆਪੁ ਗਵਾਇ ਸੇਵਾ ਕਰੇ ਤਾ ਕਿਛੁ ਪਾਏ ਮਾਨੁ ॥ aap gavaa-ay sayvaa karay taa kichh paa-ay maan. Lakini iwapo atatumika bila ya ubinafsi, basi yeye anapata utambuzi.
ਨਾਨਕ ਜਿਸ ਨੋ ਲਗਾ ਤਿਸੁ ਮਿਲੈ ਲਗਾ ਸੋ ਪਰਵਾਨੁ ॥੧॥ naanak jis no lagaa tis milai lagaa so parvaan. ||1|| Ee Nanak, iwapo yeye ataunganishwa na yule ambaye ameambatishwa, kiambatisho chake kinakubalika.
ਮਹਲਾ ੨ ॥ mehlaa 2. Salok, Guru wa Pili:
ਜੋ ਜੀਇ ਹੋਇ ਸੁ ਉਗਵੈ ਮੁਹ ਕਾ ਕਹਿਆ ਵਾਉ ॥ jo jee-ay ho-ay so ugvai muh kaa kahi-aa vaa-o. Chochote kilicho akilini kinakuwa dhahiri usoni; maneno yanayozungumzwa tu yanaweza kuwa usemi wa uongo.
ਬੀਜੇ ਬਿਖੁ ਮੰਗੈ ਅੰਮ੍ਰਿਤੁ ਵੇਖਹੁ ਏਹੁ ਨਿਆਉ ॥੨॥ beejay bikh mangai amrit vaykhhu ayhu ni-aa-o. ||2|| Tazama aina ya haki mtu anayoitarajia, kwamba anapanda sumu, lakini anaulizia Nekta kama mavuno? (kutenda vitendo vibaya na kutarajia matokeo mazuri).
ਮਹਲਾ ੨ ॥ mehlaa 2. Salok, Guru wa Pili:
ਨਾਲਿ ਇਆਣੇ ਦੋਸਤੀ ਕਦੇ ਨ ਆਵੈ ਰਾਸਿ ॥ naal i-aanay dostee kaday na aavai raas. Urafiki na mtu mwenye akili ambazo hazijakomaa kamwe haufaulu.
ਜੇਹਾ ਜਾਣੈ ਤੇਹੋ ਵਰਤੈ ਵੇਖਹੁ ਕੋ ਨਿਰਜਾਸਿ ॥ jayhaa jaanai tayho vartai vaykhhu ko nirjaas. Kama ajuavyo, yeye hutenda; yeyote anaweza kujijaribia hili mwenyewe.
ਵਸਤੂ ਅੰਦਰਿ ਵਸਤੁ ਸਮਾਵੈ ਦੂਜੀ ਹੋਵੈ ਪਾਸਿ ॥ vastoo andar vasat samaavai doojee hovai paas. Kitu kimoja kinaweza kuzamishwa ndani ya kitu kingine iwapo tu kilicho ndani yake kwanza kiwekwe kando (vivyo hivyo, mtu anaweza tu kuthamini Mungu moyoni iwapo kwanza ataondoa ubinafsi na maovu akilini)
ਸਾਹਿਬ ਸੇਤੀ ਹੁਕਮੁ ਨ ਚਲੈ ਕਹੀ ਬਣੈ ਅਰਦਾਸਿ ॥ saahib saytee hukam na chalai kahee banai ardaas. Sio amri, bali ombi nyenyekevu, ambalo hufanya kazi na Bwana.
ਕੂੜਿ ਕਮਾਣੈ ਕੂੜੋ ਹੋਵੈ ਨਾਨਕ ਸਿਫਤਿ ਵਿਗਾਸਿ ॥੩॥ koorh kamaanai koorho hovai naanak sifat vigaas. ||3|| Ee Nanak, tokeo la kutenda udanganyifu ni udanganyifu, sifa ya Mungu pekee, ndiyo huleta furaha.
ਮਹਲਾ ੨ ॥ mehlaa 2. Salok, Guru wa Pili:
ਨਾਲਿ ਇਆਣੇ ਦੋਸਤੀ ਵਡਾਰੂ ਸਿਉ ਨੇਹੁ ॥ naal i-aanay dostee vadaaroo si-o nayhu. Urafiki na mtu ambaye hajakomaa, na upendo na mtu fidhuli
ਪਾਣੀ ਅੰਦਰਿ ਲੀਕ ਜਿਉ ਤਿਸ ਦਾ ਥਾਉ ਨ ਥੇਹੁ ॥੪॥ paanee andar leek ji-o tis daa thaa-o na thayhu. ||4|| Ni kama mistari iliyochorwa majini, isiyoacha alama yoyote.
ਮਹਲਾ ੨ ॥ mehlaa 2. Salok, Guru wa Pili:
ਹੋਇ ਇਆਣਾ ਕਰੇ ਕੰਮੁ ਆਣਿ ਨ ਸਕੈ ਰਾਸਿ ॥ ho-ay i-aanaa karay kamm aan na sakai raas. Iwapo mtu ambaye hajakomaa afanye kazi, yeye hawezi kuifanya vizuri.
ਜੇ ਇਕ ਅਧ ਚੰਗੀ ਕਰੇ ਦੂਜੀ ਭੀ ਵੇਰਾਸਿ ॥੫॥ jay ik aDh changee karay doojee bhee vayraas. ||5|| Hata akifanya kitu vizuri, yeye atafanya kitu kitakachofuata vibaya.
ਪਉੜੀ ॥ pa-orhee. Pauree:
ਚਾਕਰੁ ਲਗੈ ਚਾਕਰੀ ਜੇ ਚਲੈ ਖਸਮੈ ਭਾਇ ॥ chaakar lagai chaakree jay chalai khasmai bhaa-ay. Iwapo mtumishi, wakati anatoa huduma, atii Mapenzi ya Bwana wake,
ਹੁਰਮਤਿ ਤਿਸ ਨੋ ਅਗਲੀ ਓਹੁ ਵਜਹੁ ਭਿ ਦੂਣਾ ਖਾਇ ॥ hurmat tis no aglee oh vajahu bhe doonaa khaa-ay. Staha yake huongezeka, na anapokea thawabu mara dufu.
ਖਸਮੈ ਕਰੇ ਬਰਾਬਰੀ ਫਿਰਿ ਗੈਰਤਿ ਅੰਦਰਿ ਪਾਇ ॥ khasmai karay baraabaree fir gairat andar paa-ay. Lakini akijifanya kuwa sawa na Bwana wake, yeye anapata ghadhabu ya Bwana wake.
ਵਜਹੁ ਗਵਾਏ ਅਗਲਾ ਮੁਹੇ ਮੁਹਿ ਪਾਣਾ ਖਾਇ ॥ vajahu gavaa-ay aglaa muhay muhi paanaa khaa-ay. Yeye hupoteza hata mapato aliyochuma (thawabu), na kupata aibu.
ਜਿਸ ਦਾ ਦਿਤਾ ਖਾਵਣਾ ਤਿਸੁ ਕਹੀਐ ਸਾਬਾਸਿ ॥ jis daa ditaa khaavnaa tis kahee-ai saabaas. Hivyo basi, tumpongeze Mungu, ambaye tunapokea lishe yetu kutoka kwake.
ਨਾਨਕ ਹੁਕਮੁ ਨ ਚਲਈ ਨਾਲਿ ਖਸਮ ਚਲੈ ਅਰਦਾਸਿ ॥੨੨॥ naanak hukam na chal-ee naal khasam chalai ardaas. ||22|| Ee Nanak, siyo amri, bali ombi nyenyekevu linalofanya kazi na Bwana.
ਸਲੋਕੁ ਮਹਲਾ ੨ ॥ salok mehlaa 2. Salok, Guru wa Pili:
ਏਹ ਕਿਨੇਹੀ ਦਾਤਿ ਆਪਸ ਤੇ ਜੋ ਪਾਈਐ ॥ ayh kinayhee daat aapas tay jo paa-ee-ai. ni aina gani hiyo ya thawabu iwapo tutadai kwamba tuliipata kwa jitihada yetu wenyewe?


© 2025 SGGS ONLINE
error: Content is protected !!
Scroll to Top