Guru Granth Sahib Translation Project

Guru Granth Sahib Swahili Page 464

Page 464

ਵਿਸਮਾਦੁ ਪਉਣੁ ਵਿਸਮਾਦੁ ਪਾਣੀ ॥ Ninastaajabu nikitazama kwamba mahali fulani upepo unavuma na kwingine maji yanatiririka,
ਵਿਸਮਾਦੁ ਅਗਨੀ ਖੇਡਹਿ ਵਿਡਾਣੀ ॥ Inastaajabisha, jinsi moto unavyoonyesha mwonyesho wake mwenyewe wa ajabu.
ਵਿਸਮਾਦੁ ਧਰਤੀ ਵਿਸਮਾਦੁ ਖਾਣੀ ॥ Ninastaajabu kwa furaha ninapotazama dunia hii ikitunza viumbe kutoka vyanzo vyote vya uhai.
ਵਿਸਮਾਦੁ ਸਾਦਿ ਲਗਹਿ ਪਰਾਣੀ ॥ Inastaajabisha, jinsi wanadamu wanavyohusishwa katika kufurahia Baraka Zako.
ਵਿਸਮਾਦੁ ਸੰਜੋਗੁ ਵਿਸਮਾਦੁ ਵਿਜੋਗੁ ॥ Inastaajabisha mchakato ambao kwa kuupitia watu wanaunganishwa na kutenganishwa
ਵਿਸਮਾਦੁ ਭੁਖ ਵਿਸਮਾਦੁ ਭੋਗੁ ॥ Ee Mungu, ni vigumu kuamini kwamba mahali pengine kuna njaa nyingi mno na mahali pengine vitu vinafurahiwa kwa wingi.
ਵਿਸਮਾਦੁ ਸਿਫਤਿ ਵਿਸਮਾਦੁ ਸਾਲਾਹ ॥ Mahali Fulani Muumba anasifiwa na kutukuzwa,
ਵਿਸਮਾਦੁ ਉਝੜ ਵਿਸਮਾਦੁ ਰਾਹ ॥ Kwingine kuna nyika ilhali kwingine kuna njia zilizotengenezwa vizuri. Inastaajabisha tu kuona mchezo huu Wako wa ajabu.
ਵਿਸਮਾਦੁ ਨੇੜੈ ਵਿਸਮਾਦੁ ਦੂਰਿ ॥ Inastaajabisha kwamba mtu anasema kwa Wewe yu karibu; mwingine anasema kwamba Wewe upo mbali mno,
ਵਿਸਮਾਦੁ ਦੇਖੈ ਹਾਜਰਾ ਹਜੂਰਿ ॥ Wakati wengine pia wanakuona Wewe kando yao (ukienea kote).
ਵੇਖਿ ਵਿਡਾਣੁ ਰਹਿਆ ਵਿਸਮਾਦੁ ॥ Nikitazama ajabu hizi, ninastaajabishwa.
ਨਾਨਕ ਬੁਝਣੁ ਪੂਰੈ ਭਾਗਿ ॥੧॥ Ee Nanak, wale wanaoelewa ajabu hizi Zako wamebarikiwa na hatima kamili.
ਮਃ ੧ ॥ Salok, ya Guru wa Kwanza:
ਕੁਦਰਤਿ ਦਿਸੈ ਕੁਦਰਤਿ ਸੁਣੀਐ ਕੁਦਰਤਿ ਭਉ ਸੁਖ ਸਾਰੁ ॥ Chochote kinachoonekana, au chochote kinachosikika kwenye mazingira ni ajabu ya nguvu Yako. Hofu kwa heshima Yako ambayo ndiyo kiini cha amani, yote ni mchezo Wako.
ਕੁਦਰਤਿ ਪਾਤਾਲੀ ਆਕਾਸੀ ਕੁਦਰਤਿ ਸਰਬ ਆਕਾਰੁ ॥ Ni nguvu Yako, ambayo inaonyeshwa katika maeneo ya chini ya dunia na angani, na katika miundo yote ya ulimwengu.
ਕੁਦਰਤਿ ਵੇਦ ਪੁਰਾਣ ਕਤੇਬਾ ਕੁਦਰਤਿ ਸਰਬ ਵੀਚਾਰੁ ॥ Vedas, puranas, vitabu vya kisemiti na mawazo yaliyoelezwa ndani yao, yamewezekana kwa nguvu Yako.
ਕੁਦਰਤਿ ਖਾਣਾ ਪੀਣਾ ਪੈਨ੍ਹ੍ਹਣੁ ਕੁਦਰਤਿ ਸਰਬ ਪਿਆਰੁ ॥ Ni nguvu Yako iliyopo, ambayo inatenda kazi kuwezesha dhana ya kula, kunywa, kuvaa na kuhisi upendo katika viumbe vinavyoishi.
ਕੁਦਰਤਿ ਜਾਤੀ ਜਿਨਸੀ ਰੰਗੀ ਕੁਦਰਤਿ ਜੀਅ ਜਹਾਨ ॥ Kwa Nguvu Yako kunatokea spishi za aina na rangi zote; kwa Nguvu Yako viumbe vinavyoishi vya dunia vinakuwepo.
ਕੁਦਰਤਿ ਨੇਕੀਆ ਕੁਦਰਤਿ ਬਦੀਆ ਕੁਦਰਤਿ ਮਾਨੁ ਅਭਿਮਾਨੁ ॥ Hata matendo yote mazuri, maovu, staha na fedheha zote zinatendeka kulingana na Nguvu na mapenzi Yako.
ਕੁਦਰਤਿ ਪਉਣੁ ਪਾਣੀ ਬੈਸੰਤਰੁ ਕੁਦਰਤਿ ਧਰਤੀ ਖਾਕੁ ॥ Kwa Nguvu Yako upepo, maji na moto upo; kwa Nguvu Yako ardhi na vumbi ipo.
ਸਭ ਤੇਰੀ ਕੁਦਰਤਿ ਤੂੰ ਕਾਦਿਰੁ ਕਰਤਾ ਪਾਕੀ ਨਾਈ ਪਾਕੁ ॥ Ee Mungu, kila kitu kipo chini ya Nguvu Yako, Wewe ndiwe Muumba mwenye nguvu yote. Jina Lako ndilo Takatifu kabisa kwa yote.
ਨਾਨਕ ਹੁਕਮੈ ਅੰਦਰਿ ਵੇਖੈ ਵਰਤੈ ਤਾਕੋ ਤਾਕੁ ॥੨॥ Ee Nanak, Yeye anathamini uumbaji kulingana na amri Yake, na anaenea kote Yeye Mwenyewe.
ਪਉੜੀ ॥ Pauree:
ਆਪੀਨ੍ਹ੍ਹੈ ਭੋਗ ਭੋਗਿ ਕੈ ਹੋਇ ਭਸਮੜਿ ਭਉਰੁ ਸਿਧਾਇਆ ॥ Baada ya kuishi kupitia maumivu na raha za maisha, mwili wa binadamu unakuwa mrundo wa mchanga na roho inaondoka.
ਵਡਾ ਹੋਆ ਦੁਨੀਦਾਰੁ ਗਲਿ ਸੰਗਲੁ ਘਤਿ ਚਲਾਇਆ ॥ Mtu aliyenaswa katika shughuli za kidunia anapofariki, yeye anaongozwa kwa mahakama ya Hakimu wa haki.
ਅਗੈ ਕਰਣੀ ਕੀਰਤਿ ਵਾਚੀਐ ਬਹਿ ਲੇਖਾ ਕਰਿ ਸਮਝਾਇਆ ॥ Hapo, vitendo vyake vizuri na vibaya vinahesabiwa na kuelezwa kwake.
ਥਾਉ ਨ ਹੋਵੀ ਪਉਦੀਈ ਹੁਣਿ ਸੁਣੀਐ ਕਿਆ ਰੂਆਇਆ ॥ Iwapo vitendo vyake vibaya vinazidi vitendo vizuri, Yeye anapewa adhabu kali. Yeye hapati pahali pa kujificha na hakuna anayesikia vilio vyake vya uchungu.
ਮਨਿ ਅੰਧੈ ਜਨਮੁ ਗਵਾਇਆ ॥੩॥ Kutokana na ujinga yeye ameharibu maisha ya kibinadamu bure.
ਸਲੋਕ ਮਃ ੧ ॥ Salok, Guru wa Kwanza:
ਭੈ ਵਿਚਿ ਪਵਣੁ ਵਹੈ ਸਦਵਾਉ ॥ Katika hofu kwa heshima ya Mungu, upepo unaendelea kuvuma milele.
ਭੈ ਵਿਚਿ ਚਲਹਿ ਲਖ ਦਰੀਆਉ ॥ Katika hofu kwa heshima (chini ya mapenzi) ya Mungu, maelfu ya mito yanatiririka.
ਭੈ ਵਿਚਿ ਅਗਨਿ ਕਢੈ ਵੇਗਾਰਿ ॥ Katika hofu kwa heshima ya Mungu, moto unatenda kazi ulioteuliwa kufanya.
ਭੈ ਵਿਚਿ ਧਰਤੀ ਦਬੀ ਭਾਰਿ ॥ Katika hofu kwa heshima ya Mungu, dunia inahimili mzigo wa uumbaji.
ਭੈ ਵਿਚਿ ਇੰਦੁ ਫਿਰੈ ਸਿਰ ਭਾਰਿ ॥ Katika hofu kwa heshima ya Mungu (chini ya amri Yake), mfalme Indra, mungu wa mvua katika muundo wa wingu ananing’inia kichwa chini, kana kwamba linatembea kwenye kichwa chake.
ਭੈ ਵਿਚਿ ਰਾਜਾ ਧਰਮ ਦੁਆਰੁ ॥ Katika Hofu ya Mungu, Hakimu wa Haki wa Dharma anasimama mlangoni Pake.
ਭੈ ਵਿਚਿ ਸੂਰਜੁ ਭੈ ਵਿਚਿ ਚੰਦੁ ॥ Chini ya Amri Yake, jua linang’aa na mwezi unaakisi.
ਕੋਹ ਕਰੋੜੀ ਚਲਤ ਨ ਅੰਤੁ ॥ Wanasafiri mamilioni ya maili, bila mwisho.
ਭੈ ਵਿਚਿ ਸਿਧ ਬੁਧ ਸੁਰ ਨਾਥ ॥ Katika hofu kwa heshima ya Mungu (chini ya amri Yake), wanaishi Wasiddha, Buddha. Miungu-nusu na Mayogi.
ਭੈ ਵਿਚਿ ਆਡਾਣੇ ਆਕਾਸ ॥ Ni katika hofu kwa heshima Yake ambapo anga imeenezwa juu ya dunia
ਭੈ ਵਿਚਿ ਜੋਧ ਮਹਾਬਲ ਸੂਰ ॥ Katika mapenzi ya Mungu, kuna wapiganaji na mashujaa wenye nguvu mno.
ਭੈ ਵਿਚਿ ਆਵਹਿ ਜਾਵਹਿ ਪੂਰ ॥ Katika hofu kwa heshima Yake, halaiki za wanadamu na viumbe wanazaliwa na kufa.
ਸਗਲਿਆ ਭਉ ਲਿਖਿਆ ਸਿਰਿ ਲੇਖੁ ॥ Uumbaji mzima unatenda kazi chini ya hofu kwa heshima (amri) Yake.
ਨਾਨਕ ਨਿਰਭਉ ਨਿਰੰਕਾਰੁ ਸਚੁ ਏਕੁ ॥੧॥ Ee Nanak, ni Mungu wa milele asiye na muundo peke yake asiye na hofu yoyote.
ਮਃ ੧ ॥ Salok, Guru wa Kwanza:
ਨਾਨਕ ਨਿਰਭਉ ਨਿਰੰਕਾਰੁ ਹੋਰਿ ਕੇਤੇ ਰਾਮ ਰਵਾਲ ॥ Ee Nanak, ni Mungu asiye na muundo peke yake, ambaye hana hofu; maelfu ya miungu wengine hawana maana mbele Yake.
ਕੇਤੀਆ ਕੰਨ੍ਹ੍ਹ ਕਹਾਣੀਆ ਕੇਤੇ ਬੇਦ ਬੀਚਾਰ ॥ Kuna hadithi nyingi mno kuhusu Krishna, wengi sana wanaotafakari juu ya Vedas.
ਕੇਤੇ ਨਚਹਿ ਮੰਗਤੇ ਗਿੜਿ ਮੁੜਿ ਪੂਰਹਿ ਤਾਲ ॥ Waombaji wengi sana wanachezacheza, wakizunguka kwa mpigo wa ngoma.
ਬਾਜਾਰੀ ਬਾਜਾਰ ਮਹਿ ਆਇ ਕਢਹਿ ਬਾਜਾਰ ॥ Wafanya mazingaombwe wanafanya mazingaombwe yao sokoni, wakitengeneza njozi ya uongo.
ਗਾਵਹਿ ਰਾਜੇ ਰਾਣੀਆ ਬੋਲਹਿ ਆਲ ਪਤਾਲ ॥ Wanaimba kuhusu wafalme na malkia, na kusimulia hadithi zisizo na maana.
ਲਖ ਟਕਿਆ ਕੇ ਮੁੰਦੜੇ ਲਖ ਟਕਿਆ ਕੇ ਹਾਰ ॥ Wanavaa vipuli na mikufu ya bei ghali.
ਜਿਤੁ ਤਨਿ ਪਾਈਅਹਿ ਨਾਨਕਾ ਸੇ ਤਨ ਹੋਵਹਿ ਛਾਰ ॥ Ee Nanak, miili, ambayo inavalishwa vito, mwishowe inakuwa majivu.


© 2017 SGGS ONLINE
error: Content is protected !!
Scroll to Top