Guru Granth Sahib Translation Project

Guru Granth Sahib Swahili Page 463

Page 463

ਮਹਲਾ ੨ ॥ mehlaa 2. Salok, Guru wa Pili:
ਜੇ ਸਉ ਚੰਦਾ ਉਗਵਹਿ ਸੂਰਜ ਚੜਹਿ ਹਜਾਰ ॥ jay sa-o chandaa ugvahi sooraj charheh hajaar. Iwapo miezi mia moja ingetokea na jua elfu moja kupambazuka,
ਏਤੇ ਚਾਨਣ ਹੋਦਿਆਂ ਗੁਰ ਬਿਨੁ ਘੋਰ ਅੰਧਾਰ ॥੨॥ aytay chaanan hidi-aaN gur bin ghor anDhaar. ||2|| Hata na mwanga mwingi hivyo, bado kungekuwa na giza totoro ya ujinga pasipo mafundisho ya Guru. (kumaanisha kwamba haijalishi kiasi kipi cha maarifa tunaweza kupata kutoka vyanzo vingine, pasipo Guru hatuwezi kupata mwangaza wa kweli au hekima takatifu).
ਮਃ ੧ ॥ mehlaa 1. Salok, Guru wa Kwanza:
ਨਾਨਕ ਗੁਰੂ ਨ ਚੇਤਨੀ ਮਨਿ ਆਪਣੈ ਸੁਚੇਤ ॥ naanak guroo na chaytnee man aapnai suchayt. Ee Nanak, wale ambao hawamkumbuki Guru na wanaojifikiria kuwa wajanja sana.
ਛੁਟੇ ਤਿਲ ਬੂਆੜ ਜਿਉ ਸੁੰਞੇ ਅੰਦਰਿ ਖੇਤ ॥ chhutay til boo-aarh ji-o sunjay andar khayt. Hawatakikani kama mimea bandia ya ufuta inayosalia imeachwa bure shambani.
ਖੇਤੈ ਅੰਦਰਿ ਛੁਟਿਆ ਕਹੁ ਨਾਨਕ ਸਉ ਨਾਹ ॥ khaytai andar chhuti-aa kaho naanak sa-o naah. Ee Nanak, wakiachwa pweke, wanaonekana kutaabika kama ambao badala ya mmoja wana mamia ya mabwana (na hivyo basi hawana bwana wa kweli)
ਫਲੀਅਹਿ ਫੁਲੀਅਹਿ ਬਪੁੜੇ ਭੀ ਤਨ ਵਿਚਿ ਸੁਆਹ ॥੩॥ falee-ah fulee-ah bapurhay bhee tan vich su-aah. ||3|| Mimea bandia ya ufuta inaonekana kutoa maua na kunawiri lakini imejawa na majivu tu. Vivyo hivyo wale, wasiofuata mafundisho ya Guru, wamekufa kiroho licha ya kuwa wamefanikiwa.
ਪਉੜੀ ॥ pa-orhee. Pauree:
ਆਪੀਨ੍ਹ੍ਹੈ ਆਪੁ ਸਾਜਿਓ ਆਪੀਨ੍ਹ੍ਹੈ ਰਚਿਓ ਨਾਉ ॥ aapeenHai aap saaji-o aapeenHai rachi-o naa-o. Mungu alijiumba Mwenyewe, na Yeye Mwenyewe aliumba utukufu Wake.
ਦੁਯੀ ਕੁਦਰਤਿ ਸਾਜੀਐ ਕਰਿ ਆਸਣੁ ਡਿਠੋ ਚਾਉ ॥ duyee kudrat saajee-ai kar aasan ditho chaa-o. Pili, Yeye alitengeneza uumbaji; akienea katika uumbaji, Yeye anautazama kwa furaha.
ਦਾਤਾ ਕਰਤਾ ਆਪਿ ਤੂੰ ਤੁਸਿ ਦੇਵਹਿ ਕਰਹਿ ਪਸਾਉ ॥ daataa kartaa aap tooN tus dayveh karahi pasaa-o. Ee Mungu, Wewe Mwenyewe ndiye mfadhili na Muumba wa viumbe vyote, na kwa Raha Yako, Wewe unatawaza neema Yako kwao.
ਤੂੰ ਜਾਣੋਈ ਸਭਸੈ ਦੇ ਲੈਸਹਿ ਜਿੰਦੁ ਕਵਾਉ ॥ tooN jaano-ee sabhsai day laisahi jind kavaa-o. Wewe ndiwe ujuaye yote; Wewe unatoa uhai, na kuuchukua tena kwa neno Lako tu.
ਕਰਿ ਆਸਣੁ ਡਿਠੋ ਚਾਉ ॥੧॥ kar aasan ditho chaa-o. ||1|| Kwa kuenea katika uumbaji, Wewe unatazama mchezo (wa dunia) kwa shauku
ਸਲੋਕੁ ਮਃ ੧ ॥ salok mehlaa 1. Salok, Guru wa Kwanza:
ਸਚੇ ਤੇਰੇ ਖੰਡ ਸਚੇ ਬ੍ਰਹਮੰਡ ॥ sachay tayray khand sachay barahmand. Ee Mungu Mwenyezi, mabara Yako ni ya Kweli (ya Milele), na wa Kweli ni Ulimwengu Wako.
ਸਚੇ ਤੇਰੇ ਲੋਅ ਸਚੇ ਆਕਾਰ ॥ sachay tayray lo-a sachay aakaar. Ya Kweli (Milele) ni dunia Zako, na uumbaji Wako ni wa Kweli.
ਸਚੇ ਤੇਰੇ ਕਰਣੇ ਸਰਬ ਬੀਚਾਰ ॥ sachay tayray karnay sarab beechaar. Ya Kweli ni matendo Yako na fikira Zako zote.
ਸਚਾ ਤੇਰਾ ਅਮਰੁ ਸਚਾ ਦੀਬਾਣੁ ॥ sachaa tayraa amar sachaa deebaan. Ya Kweli ni Amri Yako na mahakama Yako ni ya Kweli.
ਸਚਾ ਤੇਰਾ ਹੁਕਮੁ ਸਚਾ ਫੁਰਮਾਣੁ ॥ sachaa tayraa hukam sachaa furmaan. Kweli ni Amri ya mapenzi Yako, Kweli ni Utaratibu Wako,
ਸਚਾ ਤੇਰਾ ਕਰਮੁ ਸਚਾ ਨੀਸਾਣੁ ॥ sachaa tayraa karam sachaa neesaan. Kweli ni Huruma Yako, Za Kweli ni thawabu Zako (ishara ya neema Yako).
ਸਚੇ ਤੁਧੁ ਆਖਹਿ ਲਖ ਕਰੋੜਿ ॥ sachay tuDh aakhahi lakh karorh. Mamilioni ya watu wanaotafakari kukuhusu pia ni wa kweli.
ਸਚੈ ਸਭਿ ਤਾਣਿ ਸਚੈ ਸਭਿ ਜੋਰਿ ॥ sachai sabh taan sachai sabh jor. Uumbaji wote unategemea nguvu na uweza Wako.
ਸਚੀ ਤੇਰੀ ਸਿਫਤਿ ਸਚੀ ਸਾਲਾਹ ॥ sachee tayree sifat sachee saalaah. Ya Kweli ni Sifa Yako, Kweli ni Ibada Yako.
ਸਚੀ ਤੇਰੀ ਕੁਦਰਤਿ ਸਚੇ ਪਾਤਿਸਾਹ ॥ sachee tayree kudrat sachay paatisaah. Ee Mfalme wa Kweli, uumbaji Wako unadumu milele.
ਨਾਨਕ ਸਚੁ ਧਿਆਇਨਿ ਸਚੁ ॥ naanak sach Dhi-aa-in sach. Ee Nanak, wale wanaotafakari kuhusu Yule wa Kweli kwa kujitoa kwa upendo wanakuwa wa Kweli wenyewe (wanaungana na Mungu)
ਜੋ ਮਰਿ ਜੰਮੇ ਸੁ ਕਚੁ ਨਿਕਚੁ ॥੧॥ jo mar jammay so kach nikach. ||1|| Lakini wale wanaopitia mzunguko wa kuzaliwa na kufa wananaswa katika udanganyifu na hawawezi kuungana na Mungu.
ਮਃ ੧ ॥ mehlaa 1. Salok, Guru wa Kwanza:
ਵਡੀ ਵਡਿਆਈ ਜਾ ਵਡਾ ਨਾਉ ॥ vadee vadi-aa-ee jaa vadaa naa-o. Ukuu wake ni mkuu, ni mkuu kama Utukufu Wake.
ਵਡੀ ਵਡਿਆਈ ਜਾ ਸਚੁ ਨਿਆਉ ॥ vadee vadi-aa-ee jaa sach ni-aa-o. Ukuu wake ni mkuu, ni wa kweli kama haki Yake.
ਵਡੀ ਵਡਿਆਈ ਜਾ ਨਿਹਚਲ ਥਾਉ ॥ vadee vadi-aa-ee jaa nihchal thaa-o. Ukuu wake ni mkuu, unaodumu kama makao Yake.
ਵਡੀ ਵਡਿਆਈ ਜਾਣੈ ਆਲਾਉ ॥ vadee vadi-aa-ee jaanai aalaa-o. Ukuu wake ni mkuu, kama Yeye anavyofahamu maombi yetu.
ਵਡੀ ਵਡਿਆਈ ਬੁਝੈ ਸਭਿ ਭਾਉ ॥ vadee vadi-aa-ee bujhai sabh bhaa-o. Mkuu ni utukufu Wake, kama Yeye anavyoelewa hisia zetu zote.
ਵਡੀ ਵਡਿਆਈ ਜਾ ਪੁਛਿ ਨ ਦਾਤਿ ॥ vadee vadi-aa-ee jaa puchh na daat. Mkuu ni ukuu Wake, kama Yeye anavyotoa bila kuulizwa.
ਵਡੀ ਵਡਿਆਈ ਜਾ ਆਪੇ ਆਪਿ ॥ vadee vadi-aa-ee jaa aapay aap. Mkuu ni utukufu Wake, kama Yeye Mwenyewe alivyo vyote katika vyote.
ਨਾਨਕ ਕਾਰ ਨ ਕਥਨੀ ਜਾਇ ॥ naanak kaar na kathnee jaa-ay. Ee Nanak, vitendo Vyake haviwezi kuelezwa.
ਕੀਤਾ ਕਰਣਾ ਸਰਬ ਰਜਾਇ ॥੨॥ keetaa karnaa sarab rajaa-ay. ||2|| Chochote alichokifanya, au atakachofanya, vyote ni kwa Mapenzi Yake Mwenyewe.
ਮਹਲਾ ੨ ॥ mehlaa 2. Salok, Guru wa Pili:
ਇਹੁ ਜਗੁ ਸਚੈ ਕੀ ਹੈ ਕੋਠੜੀ ਸਚੇ ਕਾ ਵਿਚਿ ਵਾਸੁ ॥ ih jag sachai kee hai koth-rhee sachay kaa vich vaas. Dunia hii ni makao ya Mungu wa Milele na Yeye anaishi ndani yake.
ਇਕਨ੍ਹ੍ਹਾ ਹੁਕਮਿ ਸਮਾਇ ਲਏ ਇਕਨ੍ਹ੍ਹਾ ਹੁਕਮੇ ਕਰੇ ਵਿਣਾਸੁ ॥ iknHaa hukam samaa-ay la-ay iknHaa hukmay karay vinaas. Kwa Amri Yake, wengine wanaunganishwa na Yeye, na wengine, kwa Amri Yake, wanaangamizwa.
ਇਕਨ੍ਹ੍ਹਾ ਭਾਣੈ ਕਢਿ ਲਏ ਇਕਨ੍ਹ੍ਹਾ ਮਾਇਆ ਵਿਚਿ ਨਿਵਾਸੁ ॥ iknHaa bhaanai kadh la-ay iknHaa maa-i-aa vich nivaas. Wengine, kwa Mapenzi Yake, wanaokolewa kutoka kwa viambatisho vya kidunia, wakati wengine wanafanywa wabaki wamezama katika hivyo.
ਏਵ ਭਿ ਆਖਿ ਨ ਜਾਪਈ ਜਿ ਕਿਸੈ ਆਣੇ ਰਾਸਿ ॥ ayv bhe aakh na jaap-ee je kisai aanay raas. Hakuna mtu anayeweza kusema nani ataokolewa kutoka kwa viambatisho vya kidunia.
ਨਾਨਕ ਗੁਰਮੁਖਿ ਜਾਣੀਐ ਜਾ ਕਉ ਆਪਿ ਕਰੇ ਪਰਗਾਸੁ ॥੩॥ naanak gurmukh jaanee-ai jaa ka-o aap karay pargaas. ||3|| Ee Nanak, mfuasi huyo pekee wa Guru anakuja kujua kuhusu siri hii ambaye Yeye anamwangazia kwa maarifa maTakatifu.
ਪਉੜੀ ॥ pa-orhee. Pauree:
ਨਾਨਕ ਜੀਅ ਉਪਾਇ ਕੈ ਲਿਖਿ ਨਾਵੈ ਧਰਮੁ ਬਹਾਲਿਆ ॥ naanak jee-a upaa-ay kai likh naavai Dharam bahaali-aa. Ee Nanak, aliyeumba roho, Mungu ameteua hakimu wa haki arekodi nakala za vitendo vyao.
ਓਥੈ ਸਚੇ ਹੀ ਸਚਿ ਨਿਬੜੈ ਚੁਣਿ ਵਖਿ ਕਢੇ ਜਜਮਾਲਿਆ ॥ othai sachay hee sach nibrhai chun vakh kadhay jajmaali-aa. Hapo, Wanadamu wanahukumiwa tu kwa msingi wa ukweli na ukweli tu; waongo (waovu) wanatiwa alama na kutenganishwa na walio wa kweli.
ਥਾਉ ਨ ਪਾਇਨਿ ਕੂੜਿਆਰ ਮੁਹ ਕਾਲ੍ਹ੍ਹੈ ਦੋਜਕਿ ਚਾਲਿਆ ॥ thaa-o na paa-in koorhi-aar muh kaalHai dojak chaali-aa. Wale wasio wa kweli hawapati nafasi katika mahakama ya Mungu na wanaondoshwa ili wateseke katika fedheha kubwa.
ਤੇਰੈ ਨਾਇ ਰਤੇ ਸੇ ਜਿਣਿ ਗਏ ਹਾਰਿ ਗਏ ਸਿ ਠਗਣ ਵਾਲਿਆ ॥ tayrai naa-ay ratay say jin ga-ay haar ga-ay se thagan vaali-aa. Wale ambao wamepenyezwa na upendo wa Jina Lako huibuka washindi, wakati waongo wanapoteza mchezo wa maisha.
ਲਿਖਿ ਨਾਵੈ ਧਰਮੁ ਬਹਾਲਿਆ ॥੨॥ likh naavai Dharam bahaali-aa. ||2|| Ee Mungu, Wewe umeteua Hakimu wa Haki kurekodi nakala za vitendo vya wanadamu.
ਸਲੋਕ ਮਃ ੧ ॥ salok mehlaa 1. Salok, Guru wa Kwanza:
ਵਿਸਮਾਦੁ ਨਾਦ ਵਿਸਮਾਦੁ ਵੇਦ ॥ vismaad naad vismaad vayd. Inastaajabisha mikondo mingi ya sauti, yanastaajabisha maarifa ya Vedas.
ਵਿਸਮਾਦੁ ਜੀਅ ਵਿਸਮਾਦੁ ਭੇਦ ॥ vismaad jee-a vismaad bhayd. Vizuri ni vuimbe, nzuri ni spishi.
ਵਿਸਮਾਦੁ ਰੂਪ ਵਿਸਮਾਦੁ ਰੰਗ ॥ vismaad roop vismaad rang. Miundo ni mizuri, na rangi ni nzuri.
ਵਿਸਮਾਦੁ ਨਾਗੇ ਫਿਰਹਿਜੰਤ ॥ vismaad naagay fireh jant. Kwa kutazama viumbe wengi mno wakizurura uchi, nimo katika hali ya kustaajabu.


© 2025 SGGS ONLINE
error: Content is protected !!
Scroll to Top