Guru Granth Sahib Translation Project

Guru Granth Sahib Swahili Page 2

Page 2

ਗਾਵੈ ਕੋ ਵੇਖੈ ਹਾਦਰਾ ਹਦੂਰਿ ॥ gaavai ko vaykhai haadraa hadoor. Wengine wanaimba sifa za Mungu wakimwona kila mahali.
ਕਥਨਾ ਕਥੀ ਨ ਆਵੈ ਤੋਟਿ ॥ kathnaa kathee na aavai tot. Wengi wanajaribu kuelezea fadhila za Mungu, lakini hakuna mwisho wa fadhila zake.
ਕਥਿ ਕਥਿ ਕਥੀ ਕੋਟੀ ਕੋਟਿ ਕੋਟਿ ॥ kath kath kathee kotee kot kot. Ingawa mamilioni wamejaribu kuelezea fadhila Zake mamilioni ya mara.
ਦੇਦਾ ਦੇ ਲੈਦੇ ਥਕਿ ਪਾਹਿ ॥ daydaa day laiday thak paahi. Mwenyezi Mungu anaendelea kutoa, ilhali wale wanaopokea wanachoka kupokea.
ਜੁਗਾ ਜੁਗੰਤਰਿ ਖਾਹੀ ਖਾਹਿ ॥ jugaa jugantar khaahee khaahi. Viumbe wote wamekuwa wakitumia zawadi Zake katika enzi zote.
ਹੁਕਮੀ ਹੁਕਮੁ ਚਲਾਏ ਰਾਹੁ ॥ hukmee hukam chalaa-ay raahu. Kwa amri Yake, Mungu, kamanda mkuu, anaendesha ulimwengu kwenye njia maalum.
ਨਾਨਕ ਵਿਗਸੈ ਵੇਪਰਵਾਹੁ ॥੩॥ naanak vigsai vayparvaahu. ||3|| O Nanak, Mungu daima hana wasiwasi na ni mwenye furaha.
ਸਾਚਾ ਸਾਹਿਬੁ ਸਾਚੁ ਨਾਇ ਭਾਖਿਆ ਭਾਉ ਅਪਾਰੁ ॥ saachaa saahib saach naa-ay bhaakhi-aa bhaa-o apaar. Mungu ni wa milele na ndivyo ilivyo haki Yake, lugha Yake ni ile ya upendo na hana mwisho.
ਆਖਹਿ ਮੰਗਹਿ ਦੇਹਿ ਦੇਹਿ ਦਾਤਿ ਕਰੇ ਦਾਤਾਰੁ ॥ aakhahi mangahi dayhi dayhi daat karay daataar. Tunamwomba zaidi na zaidi na Mungu mwenye nguvu anaendelea kutoa.
ਫੇਰਿ ਕਿ ਅਗੈ ਰਖੀਐ ਜਿਤੁ ਦਿਸੈ ਦਰਬਾਰੁ ॥ fayr ke agai rakhee-ai jit disai darbaar. Basi tunapaswa kumpa nini ili tuweze kuona uwepo wake?
ਮੁਹੌ ਕਿ ਬੋਲਣੁ ਬੋਲੀਐ ਜਿਤੁ ਸੁਣਿ ਧਰੇ ਪਿਆਰੁ ॥ muhou ke bolan bolee-ai jit sun Dharay pi-aar. Ni maneno gani tunayoweza kuzungumza ili kuchochea upendo Wake?
ਅੰਮ੍ਰਿਤ ਵੇਲਾ ਸਚੁ ਨਾਉ ਵਡਿਆਈ ਵੀਚਾਰੁ ॥ amrit vaylaa sach naa-o vadi-aa-ee veechaar. Katika masaa ya kibinafsi kabla ya asubuhi, soma Jina la Kweli, na kutafakari fadhila zake za utukufu.
ਕਰਮੀ ਆਵੈ ਕਪੜਾ ਨਦਰੀ ਮੋਖੁ ਦੁਆਰੁ ॥ karmee aavai kaprhaa nadree mokh du-aar. Mwili wa mwanadamu unapatikana kupitia matendo mema lakini ukombozi kutoka kwa maovu unafikiwa kupitia neema Yake.
ਨਾਨਕ ਏਵੈ ਜਾਣੀਐ ਸਭੁ ਆਪੇ ਸਚਿਆਰੁ ॥੪॥ naanak ayvai jaanee-ai sabh aapay sachiaar. ||4|| O Nanak, kwa njia hii tunatambua kwamba Mungu ni wa milele, yupo kila mahali na anajidumisha Mwenyewe.
ਥਾਪਿਆ ਨ ਜਾਇ ਕੀਤਾ ਨ ਹੋਇ ॥ thaapi-aa na jaa-ay keetaa na ho-ay. Hawezi kuwekwa (kufungwa), Hawezi kuumbwa.
ਆਪੇ ਆਪਿ ਨਿਰੰਜਨੁ ਸੋਇ ॥ aapay aap niranjan so-ay. Mungu asiye na makosa alijifanya kuwepo Mwenyewe.
ਜਿਨਿ ਸੇਵਿਆ ਤਿਨਿ ਪਾਇਆ ਮਾਨੁ ॥ jin sayvi-aa tin paa-i-aa maan. Mtu aliyemkumbuka kwa ibada ya upendo, alipokea heshima.
ਨਾਨਕ ਗਾਵੀਐ ਗੁਣੀ ਨਿਧਾਨੁ ॥ naanak gaavee-ai gunee niDhaan. O Nanak, hebu tuimbe sifa za Mungu, hazina ya fadhila.
ਗਾਵੀਐ ਸੁਣੀਐ ਮਨਿ ਰਖੀਐ ਭਾਉ ॥ gaavee-ai sunee-ai man rakhee-ai bhaa-o. Hebu tuimbe na kusikiliza matendo Yake, na tuuweke upendo Wake moyoni mwetu.
ਦੁਖੁ ਪਰਹਰਿ ਸੁਖੁ ਘਰਿ ਲੈ ਜਾਇ ॥ dukh parhar sukh ghar lai jaa-ay. Mtu anayefanya hivyo, huondoa huzuni yake na hupata amani moyoni mwake.
ਗੁਰਮੁਖਿ ਨਾਦੰ ਗੁਰਮੁਖਿ ਵੇਦੰ ਗੁਰਮੁਖਿ ਰਹਿਆ ਸਮਾਈ ॥ gurmukh naadaN gurmukh vaydaN gurmukh rahi-aa samaa-ee. Kupitia kwa Guru tunapata neno la kimungu, kupitia kwa Guru tunapata maarifa ya kimungu na kupitia kwa Guru tunatambua kwamba Mungu anaenea kote.
ਗੁਰੁ ਈਸਰੁ ਗੁਰੁ ਗੋਰਖੁ ਬਰਮਾ ਗੁਰੁ ਪਾਰਬਤੀ ਮਾਈ ॥ gur eesar gur gorakh barmaa gur paarbatee maa-ee. Kwetu, Guru mwenyewe ni Bwana Shiva, Vishnu, Brahma na Parbati.
ਜੇ ਹਉ ਜਾਣਾ ਆਖਾ ਨਾਹੀ ਕਹਣਾ ਕਥਨੁ ਨ ਜਾਈ ॥ jay ha-o jaanaa aakhaa naahee kahnaa kathan na jaa-ee. Hata kama nitamtambua Mungu, Sitaweza kumwelezea kwa sababu Yeye hawezi kuelezewa kwa maneno.
ਗੁਰਾ ਇਕ ਦੇਹਿ ਬੁਝਾਈ ॥ guraa ik dayhi bujhaa-ee. O Guru wangu, tafadhali nibariki na uelewa huu kwamba:
ਸਭਨਾ ਜੀਆ ਕਾ ਇਕੁ ਦਾਤਾ ਸੋ ਮੈ ਵਿਸਰਿ ਨ ਜਾਈ ॥੫॥ sabhnaa jee-aa kaa ik daataa so mai visar na jaa-ee. ||5|| Siwezi kamwe kumsahau Mungu, yeye pekee atoaye kwa viumbe wote walio hai.
ਤੀਰਥਿ ਨਾਵਾ ਜੇ ਤਿਸੁ ਭਾਵਾ ਵਿਣੁ ਭਾਣੇ ਕਿ ਨਾਇ ਕਰੀ ॥ tirath naavaa jay tis bhaavaa vin bhaanay ke naa-ay karee. Nitaoga katika maeneo ya hiji tu ikiwa inampendeza Mungu; bila kumpendeza Mungu, ina haja gani nifanye ibada hiyo ya kuoga?
ਜੇਤੀ ਸਿਰਠਿ ਉਪਾਈ ਵੇਖਾ ਵਿਣੁ ਕਰਮਾ ਕਿ ਮਿਲੈ ਲਈ ॥ jaytee sirath upaa-ee vaykhaa vin karmaa ke milai la-ee. Ninapoangalia ulimwengu wote ulioumbwa na Yeye, (Ninatambua kwamba) hakuna kitu kinachoweza kupatikana bila baraka Yake.
ਮਤਿ ਵਿਚਿ ਰਤਨ ਜਵਾਹਰ ਮਾਣਿਕ ਜੇ ਇਕ ਗੁਰ ਕੀ ਸਿਖ ਸੁਣੀ ॥ mat vich ratan javaahar maanik jay ik gur kee sikh sunee. Akili inakuwa tajiri na maarifa ya thamani ya kimungu mtu anaposikiliza mafundisho ya Guru hata mara moja.
ਗੁਰਾ ਇਕ ਦੇਹਿ ਬੁਝਾਈ ॥ guraa ik dayhi bujhaa-ee. Ee Guru wangu, tafadhali nibariki kwa uelewa huu kwamba;
ਸਭਨਾ ਜੀਆ ਕਾ ਇਕੁ ਦਾਤਾ ਸੋ ਮੈ ਵਿਸਰਿ ਨ ਜਾਈ ॥੬॥ sabhnaa jee-aa kaa ik daataa so mai visar na jaa-ee. ||6|| Siwezi kamwe kumsahau Mungu, anayewapa viumbe wote walio hai.
ਜੇ ਜੁਗ ਚਾਰੇ ਆਰਜਾ ਹੋਰ ਦਸੂਣੀ ਹੋਇ ॥ jay jug chaaray aarjaa hor dasoonee ho-ay. hata mtu akiishi enzi zote nne, au hata mara kumi zaidi,
ਨਵਾ ਖੰਡਾ ਵਿਚਿ ਜਾਣੀਐ ਨਾਲਿ ਚਲੈ ਸਭੁ ਕੋਇ ॥ navaa khanda vich jaanee-ai naal chalai sabh ko-ay. Na hata kama anajulikana duniani kote na kuheshimiwa na kila mtu,
ਚੰਗਾ ਨਾਉ ਰਖਾਇ ਕੈ ਜਸੁ ਕੀਰਤਿ ਜਗਿ ਲੇਇ ॥ changa naa-o rakhaa-ay kai jas keerat jag lay-ay. awe na sifa nzuri na umaarufu duniani kote,
ਜੇ ਤਿਸੁ ਨਦਰਿ ਨ ਆਵਈ ਤ ਵਾਤ ਨ ਪੁਛੈ ਕੇ ॥ jay tis nadar na aavee ta vaat na puchhai kay. Bado hakuna mtu ambaye angejali kuhusu mtu huyo bila neema ya Mungu.
ਕੀਟਾ ਅੰਦਰਿ ਕੀਟੁ ਕਰਿ ਦੋਸੀ ਦੋਸੁ ਧਰੇ ॥ keetaa andar keet kar dosee dos Dharay. Mtu kama huyo anachukuliwa kuwa chini sana, (kama mnyoo mdogo), na hata wenye dhambi watachukizwa naye.
ਨਾਨਕ ਨਿਰਗੁਣਿ ਗੁਣੁ ਕਰੇ ਗੁਣਵੰਤਿਆ ਗੁਣੁ ਦੇ ॥ naanak nirgun gun karay gunvanti-aa gun day. Ee Nanak, Mungu anaweza kubariki hata watu wasio wema kwa fadhila, na anaweza kuwapa fadhila zaidi walio wema.
ਤੇਹਾ ਕੋਇ ਨ ਸੁਝਈ ਜਿ ਤਿਸੁ ਗੁਣੁ ਕੋਇ ਕਰੇ ॥੭॥ tayhaa ko-ay na sujh-ee je tis gun ko-ay karay. ||7|| Siwezi hata kufikiria mtu yeyote isipokuwa Mungu ambaye anaweza kutoa fadhila kwa wasio na wema.
ਸੁਣਿਐ ਸਿਧ ਪੀਰ ਸੁਰਿ ਨਾਥ ॥ suni-ai siDh peer sur naath. Kwa kusikiliza sifa za Mungu hata watu wa kawaida wanapata hadhi ya Sidhas (yogi), Peers (viongozi wa kidini wa Kiislamu), miungu, na Naathu (viongozi wa yoga).
ਸੁਣਿਐ ਧਰਤਿ ਧਵਲ ਆਕਾਸ ॥ suni-ai Dharat Dhaval aakaas. Kwa kusikiliza Naam (mtu anaelewa siri ya) dunia, na ndume halisi (au nguvu), inayosaidia dunia na angani.
ਸੁਣਿਐ ਦੀਪ ਲੋਅ ਪਾਤਾਲ ॥ suni-ai deep lo-a paataal. Kwa kusikiliza Naam, mtu anaelewa kuwa Mungu anazingatia mabara yote, ulimwengu, na mikoa ya chini.
ਸੁਣਿਐ ਪੋਹਿ ਨ ਸਕੈ ਕਾਲੁ ॥ suni-ai pohi na sakai kaal. Kwa kusikiliza sifa za Mungu, mtu haogopi kifo.
ਨਾਨਕ ਭਗਤਾ ਸਦਾ ਵਿਗਾਸੁ ॥ naanak bhagtaa sadaa vigaas. Ee Nanak, wanaomwabudu huwa katika furaha na raha milele.
ਸੁਣਿਐ ਦੂਖ ਪਾਪ ਕਾ ਨਾਸੁ ॥੮॥ suni-ai dookh paap kaa naas. ||8|| Kwa Kusikiliza sifa za Mungu, huzuni na dhambi zote zinafutwa. |8||
ਸੁਣਿਐ ਈਸਰੁ ਬਰਮਾ ਇੰਦੁ ॥ suni-ai eesar barmaa ind. Kwa Kusikiliza Naam, mtu hupata sifa za Mungu kama ile za Shiva, Brahma na Indra.
ਸੁਣਿਐ ਮੁਖਿ ਸਾਲਾਹਣ ਮੰਦੁ ॥ suni-ai mukh saalaahan mand. Kwa kusikiliza Naam, hata wenye dhambi wanapata nuru na kuanza kuimba sifa za Mungu.
ਸੁਣਿਐ ਜੋਗ ਜੁਗਤਿ ਤਨਿ ਭੇਦ ॥ suni-ai jog jugat tan bhayd. Kwa kusikiliza Naam, mtu anaanza kuelewa siri za kuungana na Mungu, na siri za mwili wa binadamu.
ਸੁਣਿਐ ਸਾਸਤ ਸਿਮ੍ਰਿਤਿ ਵੇਦ ॥ suni-ai saasat simrit vayd. Kwa kusikiliza Jina la Mungu, mtu anapata maarifa ya kiroho yaliyoelezwa katika maandiko takatifu.
ਨਾਨਕ ਭਗਤਾ ਸਦਾ ਵਿਗਾਸੁ ॥ naanak bhagtaa sadaa vigaas. Ee Nanak, waabudu wa Mungu wako milele katika furaha.


© 2025 SGGS ONLINE
error: Content is protected !!
Scroll to Top