Guru Granth Sahib Translation Project

Guru Granth Sahib Swahili Page 291

Page 291

ਆਪਨ ਖੇਲੁ ਆਪਿ ਵਰਤੀਜਾ ॥ aapan khayl aap varteejaa. Yeye Mwenyewe ameupanga mchezo wake mwenyewe,
ਨਾਨਕ ਕਰਨੈਹਾਰੁ ਨ ਦੂਜਾ ॥੧॥ naanak karnaihaar na doojaa. ||1|| Ee Nanak, hakuna Muumba mwengine.
ਜਬ ਹੋਵਤ ਪ੍ਰਭ ਕੇਵਲ ਧਨੀ ॥ jab hovat parabh kayval Dhanee. Kulipokuwa na Mungu tu, Bwana,
ਤਬ ਬੰਧ ਮੁਕਤਿ ਕਹੁ ਕਿਸ ਕਉ ਗਨੀ ॥ tab banDh mukat kaho kis ka-o ganee. Basi nani alifikiriwa kuwa ameambatishwa kwa Maya au kukombolewa kutoka kwa Maya?
ਜਬ ਏਕਹਿ ਹਰਿ ਅਗਮ ਅਪਾਰ ॥ jab aykeh har agam apaar. Wakati kulikuwa na Mungu pekee, Asiyefahamika na Asiye na mwisho,
ਤਬ ਨਰਕ ਸੁਰਗ ਕਹੁ ਕਉਨ ਅਉਤਾਰ ॥ tab narak surag kaho ka-un a-utaar. Basi ni nani aliyeingia jehanamu, na ni nani aliyeingia mbinguni?
ਜਬ ਨਿਰਗੁਨ ਪ੍ਰਭ ਸਹਜ ਸੁਭਾਇ ॥ jab nirgun parabh sahj subhaa-ay. Wakati Mungu alikuwa bila sifa, katika utulivu kamili,
ਤਬ ਸਿਵ ਸਕਤਿ ਕਹਹੁ ਕਿਤੁ ਠਾਇ ॥ tab siv sakat kahhu kit thaa-ay. basi (shiva) roho ilikuwa wapi na (shakti) ilikuwa wapi
ਜਬ ਆਪਹਿ ਆਪਿ ਅਪਨੀ ਜੋਤਿ ਧਰੈ ॥ jab aapeh aap apnee jot Dharai. Wakati aliushika Mwanga wake Mwenyewe kwake Mwenyewe,
ਤਬ ਕਵਨ ਨਿਡਰੁ ਕਵਨ ਕਤ ਡਰੈ ॥ tab kavan nidar kavan kat darai. Basi nani aliyekuwa bila woga, na nani aliyeogopa yeyote?
ਆਪਨ ਚਲਿਤ ਆਪਿ ਕਰਨੈਹਾਰ ॥ aapan chalit aap karnaihaar. Yeye Mwenyewe ndiye Mwigizaji wa michezo yake mwenyewe;
ਨਾਨਕ ਠਾਕੁਰ ਅਗਮ ਅਪਾਰ ॥੨॥ naanak thaakur agam apaar. ||2|| Ee Nanak, Bwana Mkuu hawezi Kufahamika wala hana mwisho.
ਅਬਿਨਾਸੀ ਸੁਖ ਆਪਨ ਆਸਨ ॥ abhinaasee sukh aapan aasan. Wakati Mungu asiyeweza kufa alizama katika hali yake mwenyewe ya amani na utulivu,
ਤਹ ਜਨਮ ਮਰਨ ਕਹੁ ਕਹਾ ਬਿਨਾਸਨ ॥ tah janam maran kaho kahaa binaasan. Basi kuzaliwa, kufa na maangamizi yalikuwa wapi?
ਜਬ ਪੂਰਨ ਕਰਤਾ ਪ੍ਰਭੁ ਸੋਇ ॥ jab pooran kartaa parabh so-ay. Wakati alikuwepo Mungu pekee, Muumba kamili,
ਤਬ ਜਮ ਕੀ ਤ੍ਰਾਸ ਕਹਹੁ ਕਿਸੁ ਹੋਇ ॥ tab jam kee taraas kahhu kis ho-ay. Basi nani aliyeogopa kifo?
ਜਬ ਅਬਿਗਤ ਅਗੋਚਰ ਪ੍ਰਭ ਏਕਾ ॥ jab abigat agochar parabh aykaa. Wakati kulikuwa na Mungu Mmoja pekee, asiyedhihirika na asiyeeleweka,
ਤਬ ਚਿਤ੍ਰ ਗੁਪਤ ਕਿਸੁ ਪੂਛਤ ਲੇਖਾ ॥ tab chitar gupat kis poochhat laykhaa. Basi Chittar na Gupat (malaika wa kunakili vitendo) walimuuliza nani aliyoyatenda?
ਜਬ ਨਾਥ ਨਿਰੰਜਨ ਅਗੋਚਰ ਅਗਾਧੇ ॥ jab naath niranjan agochar agaaDhay. Wakati alikuwepo tu Bwana Safi, Asiyeeleweka, Asiyefahamika,
ਤਬ ਕਉਨ ਛੁਟੇ ਕਉਨ ਬੰਧਨ ਬਾਧੇ ॥ tab ka-un chhutay ka-un banDhan baaDhay. Basi nani aliyekombolewa, na nani aliyenaswa katika vifungo vya Maya?
ਆਪਨ ਆਪ ਆਪ ਹੀ ਅਚਰਜਾ ॥ aapan aap aap hee acharjaa. Mungu huyo mzuri pekee ndiye aliye kama Yeye Mwenyewe.
ਨਾਨਕ ਆਪਨ ਰੂਪ ਆਪ ਹੀ ਉਪਰਜਾ ॥੩॥ naanak aapan roop aap hee uparjaa. ||3|| Ee Nanak, Yeye Mwenyewe ndiye aliyeumba Muundo wake Mwenyewe.
ਜਹ ਨਿਰਮਲ ਪੁਰਖੁ ਪੁਰਖ ਪਤਿ ਹੋਤਾ ॥ jah nirmal purakh purakh pat hotaa. Wakati Kiumbe Safi, Bwana wa binadamu alikuwa peke yake,
ਤਹ ਬਿਨੁ ਮੈਲੁ ਕਹਹੁ ਕਿਆ ਧੋਤਾ ॥ tah bin mail kahhu ki-aa Dhotaa. Hakukuwa na uchafu wa dhambi, hivyo kulikuwa na kipi cha kusafishwa?
ਜਹ ਨਿਰੰਜਨ ਨਿਰੰਕਾਰ ਨਿਰਬਾਨ ॥ jah niranjan nirankaar nirbaan. Wakati kulikuwa tu na Mungu safi, asiye na umbo na asiye na hamu zozote,
ਤਹ ਕਉਨ ਕਉ ਮਾਨ ਕਉਨ ਅਭਿਮਾਨ ॥ tah ka-un ka-o maan ka-un abhimaan. Basi nani aliyekuwa na kujistahi na nani aliyekuwa na ubinafsi?
ਜਹ ਸਰੂਪ ਕੇਵਲ ਜਗਦੀਸ ॥ jah saroop kayval jagdees. Wakati kulikuwa na Bwana wa Ulimwengu pekee,
ਤਹ ਛਲ ਛਿਦ੍ਰ ਲਗਤ ਕਹੁ ਕੀਸ ॥ tah chhal chhidar lagat kaho kees. Basi nani aliyechafuliwa na ulaghai na dhambi?
ਜਹ ਜੋਤਿ ਸਰੂਪੀ ਜੋਤਿ ਸੰਗਿ ਸਮਾਵੈ ॥ jah jot saroopee jot sang samaavai. Wakati udhihirisho wa Mwanga (Mungu) alizama katika Mwanga Wake Mwenyewe,
ਤਹ ਕਿਸਹਿ ਭੂਖ ਕਵਨੁ ਤ੍ਰਿਪਤਾਵੈ ॥ tah kiseh bhookh kavan tariptaavai. Basi nani aliyetamani Maya, na nani aliyeridhishwa?
ਕਰਨ ਕਰਾਵਨ ਕਰਨੈਹਾਰੁ ॥ karan karaavan karnaihaar. Muumba ndiye mtendaji wa kila kitu na Msingi wa misingi yote.
ਨਾਨਕ ਕਰਤੇ ਕਾ ਨਾਹਿ ਸੁਮਾਰੁ ॥੪॥ naanak kartay kaa naahi sumaar. ||4|| Ee Nanak, Muumba amezidi kukadiriwa
ਜਬ ਅਪਨੀ ਸੋਭਾ ਆਪਨ ਸੰਗਿ ਬਨਾਈ ॥ jab apnee sobhaa aapan sang banaa-ee. Alipoubeba Utukufu wake ndani mwake,
ਤਬ ਕਵਨ ਮਾਇ ਬਾਪ ਮਿਤ੍ਰ ਸੁਤ ਭਾਈ ॥ tab kavan maa-ay baap mitar sut bhaa-ee. Basi nani alikuwa mama, baba, mtoto au ndugu?
ਜਹ ਸਰਬ ਕਲਾ ਆਪਹਿ ਪਰਬੀਨ ॥ jah sarab kalaa aapeh parbeen. Mungu Mwenyewe alipokuwa mkuu zaidi katika nguvu zote,
ਤਹ ਬੇਦ ਕਤੇਬ ਕਹਾ ਕੋਊ ਚੀਨ ॥ tah bayd katayb kahaa ko-oo cheen. Basi alikuwepo nani akisoma Vedas na katebas (vitabu vya kidini)?
ਜਬ ਆਪਨ ਆਪੁ ਆਪਿ ਉਰਿ ਧਾਰੈ ॥ jab aapan aap aap ur Dhaarai. Wakati Yeye alijiweka Mwenyewe, kwake mwenyewe,
ਤਉ ਸਗਨ ਅਪਸਗਨ ਕਹਾ ਬੀਚਾਰੈ ॥ ta-o sagan apasgan kahaa beechaarai. Badi nani aliyefikiria ishara kuwa nzuri au mbaya?
ਜਹ ਆਪਨ ਊਚ ਆਪਨ ਆਪਿ ਨੇਰਾ ॥ jah aapan ooch aapan aap nayraa. Wakati Yeye Mwenyewe alikuwa wa juu zaidi na Mwenyewe wa chini (katika cheo),
ਤਹ ਕਉਨ ਠਾਕੁਰੁ ਕਉਨੁ ਕਹੀਐ ਚੇਰਾ ॥ tah ka-un thaakur ka-un kahee-ai chayraa. Basi nani aliyekuwa bwana, na nani aliyekuwa mtumishi?
ਬਿਸਮਨ ਬਿਸਮ ਰਹੇ ਬਿਸਮਾਦ ॥ bisman bisam rahay bismaad. Watu wanastaajabishwa na miujiza ya ajabu ya Uumbaji wako.
ਨਾਨਕ ਅਪਨੀ ਗਤਿ ਜਾਨਹੁ ਆਪਿ ॥੫॥ nanak apnee gat jaanhu aap. ||5|| Nanak anasema, Ee Mungu ni Wewe pekee unayejua hali Yako
ਜਹ ਅਛਲ ਅਛੇਦ ਅਭੇਦ ਸਮਾਇਆ ॥ jah achhal achhayd abhayd samaa-i-aa. Wakati yule Mmoja asiyeweza kudanganywa, asiyeweza kuangamia na asiyeeleweka alizama ndani mwake Mwenyewe.
ਊਹਾ ਕਿਸਹਿ ਬਿਆਪਤ ਮਾਇਆ ॥ oohaa kiseh bi-aapat maa-i-aa. Basi nani aliyeyumbishwa na Maya (vivutio vya kidunia)?
ਆਪਸ ਕਉ ਆਪਹਿ ਆਦੇਸੁ ॥ aapas ka-o aapeh aadays. Wakati Yeye alitoa heshima kwake Mwenyewe,
ਤਿਹੁ ਗੁਣ ਕਾ ਨਾਹੀ ਪਰਵੇਸੁ ॥ tihu gun kaa naahee parvays. Basi miundo tatu za Maya (nguvu, dhambi na fadhila) haikudumu.
ਜਹ ਏਕਹਿ ਏਕ ਏਕ ਭਗਵੰਤਾ ॥ jah aykeh ayk ayk bhagvantaa. Wakati kulikuwa na Mungu Mmoja, Mkuu peke yake,
ਤਹ ਕਉਨੁ ਅਚਿੰਤੁ ਕਿਸੁ ਲਾਗੈ ਚਿੰਤਾ ॥ tah ka-un achint kis laagai chintaa. Basi nani hakuwa na wasiwasi, na nani aliyehisi wasiwasi?
ਜਹ ਆਪਨ ਆਪੁ ਆਪਿ ਪਤੀਆਰਾ ॥ jah aapan aap aap patee-aaraa. Wakati Yeye alikuwa peke yake wa kumpendeza Yeye,
ਤਹ ਕਉਨੁ ਕਥੈ ਕਉਨੁ ਸੁਨਨੈਹਾਰਾ ॥ tah ka-un kathai ka-un sunnaihaaraa. Basi nani aliyekuwa hatibu na nani aliyekuwa msikilizaji?
ਬਹੁ ਬੇਅੰਤ ਊਚ ਤੇ ਊਚਾ ॥ baho bay-ant ooch tay oochaa. Yeye ni mkubwa asiye na mwisho na aliye juu zaidi ya wote.
ਨਾਨਕ ਆਪਸ ਕਉ ਆਪਹਿ ਪਹੂਚਾ ॥੬॥ naanak aapas ka-o aapeh pahoochaa. ||6|| Ee Nanak, Yeye pekee anaweza kujifahamu Mwenyewe.
ਜਹ ਆਪਿ ਰਚਿਓ ਪਰਪੰਚੁ ਅਕਾਰੁ ॥ jah aap rachi-o parpanch akaar. Wakati Mungu aliutengeneza ulimwengu huu wa muundo unaoonekana,
ਤਿਹੁ ਗੁਣ ਮਹਿ ਕੀਨੋ ਬਿਸਥਾਰੁ ॥ tihu gun meh keeno bisthaar. Alifanya dunia itii miundo mitatu yaMaya (dhambi, fadhila na nguvu).
ਪਾਪੁ ਪੁੰਨੁ ਤਹ ਭਈ ਕਹਾਵਤ ॥ paap punn tah bha-ee kahaavat. Kisha dhana ya dhambi na fadhila ikaja kuwepo.


© 2025 SGGS ONLINE
error: Content is protected !!
Scroll to Top