Page 286
ਤਾ ਕਉ ਰਾਖਤ ਦੇ ਕਰਿ ਹਾਥ ॥
taa ka-o raakhat day kar haath.
Yeye Mwenyewe anamhifadhi.
ਮਾਨਸ ਜਤਨ ਕਰਤ ਬਹੁ ਭਾਤਿ ॥
maanas jatan karat baho bhaat.
Mtu hufanya aina zote za jitihada,
ਤਿਸ ਕੇ ਕਰਤਬ ਬਿਰਥੇ ਜਾਤਿ ॥
tis kay kartab birthay jaat.
Lakini jitihada hizi zote ni bure bila mapenzi ya Mungu.
ਮਾਰੈ ਨ ਰਾਖੈ ਅਵਰੁ ਨ ਕੋਇ ॥
maarai na raakhai avar na ko-ay.
hakuna mwingine ila Mungu Mwenyewe anayeweza kuokoa au kuua.
ਸਰਬ ਜੀਆ ਕਾ ਰਾਖਾ ਸੋਇ ॥
sarab jee-aa kaa raakhaa so-ay.
Mungu ndiye Mlinzi wa viumbe vyote;
ਕਾਹੇ ਸੋਚ ਕਰਹਿ ਰੇ ਪ੍ਰਾਣੀ ॥
kaahay soch karahi ray paraanee.
Hivyo, kwa nini una wasiwasi, Ee binadamu?
ਜਪਿ ਨਾਨਕ ਪ੍ਰਭ ਅਲਖ ਵਿਡਾਣੀ ॥੫॥
jap naanak parabh alakh vidaanee. ||5||
Tafakari Ee Nanak, kuhusu Mungu huyo asiyeeleweka na wa ajabu.
ਬਾਰੰ ਬਾਰ ਬਾਰ ਪ੍ਰਭੁ ਜਪੀਐ ॥
baaraN baar baar parabh japee-ai.
Tena na tena, hebu tutafakari kumhusu Yeye,
ਪੀ ਅੰਮ੍ਰਿਤੁ ਇਹੁ ਮਨੁ ਤਨੁ ਧ੍ਰਪੀਐ ॥
pee amrit ih man tan Dharpee-ai.
na kwa kunywa dawa ya Naam, hebu tutosheleze akili yetu na hisia za mwili ( hisia za kusikia, kuona, kunusa, kugusa na kadhalika.)
ਨਾਮ ਰਤਨੁ ਜਿਨਿ ਗੁਰਮੁਖਿ ਪਾਇਆ ॥
naam ratan jin gurmukh paa-i-aa.
Mfuasi wa Guru ambaye amepata kito cha Naam,
ਤਿਸੁ ਕਿਛੁ ਅਵਰੁ ਨਾਹੀ ਦ੍ਰਿਸਟਾਇਆ ॥
tis kichh avar naahee daristaa-i-aa.
Kila mahali humwona Mungu pekee.
ਨਾਮੁ ਧਨੁ ਨਾਮੋ ਰੂਪੁ ਰੰਗੁ ॥
naam Dhan naamo roop rang.
Kwake, Jina la Mungu ni utajiri wa kweli na uzuri wa kweli.
ਨਾਮੋ ਸੁਖੁ ਹਰਿ ਨਾਮ ਕਾ ਸੰਗੁ ॥
naamo sukh har naam kaa sang.
Jina la Mungu ni starehe na mwandani wake.
ਨਾਮ ਰਸਿ ਜੋ ਜਨ ਤ੍ਰਿਪਤਾਨੇ ॥
naam ras jo jan tariptaanay.
Wale ambao wametoshelezwa na kiini cha Naam,
ਮਨ ਤਨ ਨਾਮਹਿ ਨਾਮਿ ਸਮਾਨੇ ॥
man tan naameh naam samaanay.
huweka akili zao na vitivo vya miili yao vikilowa kwa Naam.
ਊਠਤ ਬੈਠਤ ਸੋਵਤ ਨਾਮ ॥
oothat baithat sovat naam.,
Ee Nanak, sema, “Siku zote, kutafakari Jina la Mungu
ਕਹੁ ਨਾਨਕ ਜਨ ਕੈ ਸਦ ਕਾਮ ॥੬॥
kaho naanak jan kai sad kaam. ||6||
Jina la Mungu linakuwa mwito endelevu wa waja wa Mungu.” ||6||
ਬੋਲਹੁ ਜਸੁ ਜਿਹਬਾ ਦਿਨੁ ਰਾਤਿ ॥
bolhu jas jihbaa din raat.
Mchana na usiku, tumia ulimi uliopewa na Mungu kutamka sifa zake.
ਪ੍ਰਭਿ ਅਪਨੈ ਜਨ ਕੀਨੀ ਦਾਤਿ ॥
parabh apnai jan keenee daat.
Tuzo hii ya kumsifu Yeye inatolewa na Mungu Mwenyewe kwa watumishi wake.
ਕਰਹਿ ਭਗਤਿ ਆਤਮ ਕੈ ਚਾਇ ॥
karahi bhagat aatam kai chaa-ay.
Watawa wanafanya ibada ya ujitoaji kwa upendo wa dhati,
ਪ੍ਰਭ ਅਪਨੇ ਸਿਉ ਰਹਹਿ ਸਮਾਇ ॥
parabh apnay si-o raheh samaa-ay.
Na hivyo wanabaki wamezama katika Mungu.
ਜੋ ਹੋਆ ਹੋਵਤ ਸੋ ਜਾਨੈ ॥
jo ho-aa hovat so jaanai.
Mtawa anaelewa na kuamini mapenzi ya Mungu kwa vyote vilivyotendeka awali na kinachotendeka wakati uliopo.
ਪ੍ਰਭ ਅਪਨੇ ਕਾ ਹੁਕਮੁ ਪਛਾਨੈ ॥
parabh apnay kaa hukam pachhaanai.
Mtawa anaelewa na kuamini mapenzi ya Mungu kwa vyote
ਤਿਸ ਕੀ ਮਹਿਮਾ ਕਉਨ ਬਖਾਨਉ ॥
tis kee mahimaa ka-un bakhaana-o.
Ni fadhila zipi za mtawa kama huyo nitakazoelezea?
ਤਿਸ ਕਾ ਗੁਨੁ ਕਹਿ ਏਕ ਨ ਜਾਨਉ ॥
tis kaa gun kahi ayk na jaan-o.
Sijui jinsi ya kueleza hata moja ya sifa zake.
ਆਠ ਪਹਰ ਪ੍ਰਭ ਬਸਹਿ ਹਜੂਰੇ ॥
aath pahar parabh baseh hajooray.
Wale wanaoishi katika uwepo wa Mungu saa ishirini na nne kwa siku,
ਕਹੁ ਨਾਨਕ ਸੇਈ ਜਨ ਪੂਰੇ ॥੭॥
kaho nanak say-ee jan pooray. ||7||
sema Ee Nanak, “Hao ni watawa kamili”.
ਮਨ ਮੇਰੇ ਤਿਨ ਕੀ ਓਟ ਲੇਹਿ ॥
man mayray tin kee ot layhi.
Ee akili yangu, tafuta ulinzi wa wale wanaoishi katika uwepo wa Mungu;
ਮਨੁ ਤਨੁ ਅਪਨਾ ਤਿਨ ਜਨ ਦੇਹਿ ॥
man tan apnaa tin jan deh.
Na uweke wakfu akili yako na vitivo vya mwili kwa watawa hao.
ਜਿਨਿ ਜਨਿ ਅਪਨਾ ਪ੍ਰਭੂ ਪਛਾਤਾ ॥
jin jan apnaa parabhoo pachhaataa.
Mtawa ambaye amemtambua Mungu,
ਸੋ ਜਨੁ ਸਰਬ ਥੋਕ ਕਾ ਦਾਤਾ ॥
so jan sarab thok kaa daataa.
anakuwa mfadhili wa vitu vyote.
ਤਿਸ ਕੀ ਸਰਨਿ ਸਰਬ ਸੁਖ ਪਾਵਹਿ ॥
tis kee saran sarab sukh paavahi.
Katika pahali pake patakatifu, starehe zote zinapatikana.
ਤਿਸ ਕੈ ਦਰਸਿ ਸਭ ਪਾਪ ਮਿਟਾਵਹਿ ॥
tis kai daras sabh paap mitaaveh.
Kwa kuwa na maono ya mtawa kama huyo, utaondoa dhambi zote.
ਅਵਰ ਸਿਆਨਪ ਸਗਲੀ ਛਾਡੁ ॥
avar si-aanap saglee chhaad.
Ukane ujanja mwingine wote,
ਤਿਸੁ ਜਨ ਕੀ ਤੂ ਸੇਵਾ ਲਾਗੁ ॥
tis jan kee too sayvaa laag.
Na ujisajili kwa huduma ya mtawa kama huyo.
ਆਵਨੁ ਜਾਨੁ ਨ ਹੋਵੀ ਤੇਰਾ ॥
aavan jaan na hovee tayraa.
mzunguko wako wa kuzaliwa na kufa utatamatika.
ਨਾਨਕ ਤਿਸੁ ਜਨ ਕੇ ਪੂਜਹੁ ਸਦ ਪੈਰਾ ॥੮॥੧੭॥
nanak tis jan kay poojahu sad pairaa. ||8||17||
Ee Nanak, kwa unyoofu, fuata daima ushauri wa mtawa kama huyo wa Mungu
ਸਲੋਕੁ ॥
salok.
Shalok:
ਸਤਿ ਪੁਰਖੁ ਜਿਨਿ ਜਾਨਿਆ ਸਤਿਗੁਰੁ ਤਿਸ ਕਾ ਨਾਉ ॥
sat purakh jin jaani-aa satgur tis kaa naa-o.
Yule ambaye amemgundua Mungu wa Kweli ambaye yupo kila mahali, anaitwa Guru wa Kweli.
ਤਿਸ ਕੈ ਸੰਗਿ ਸਿਖੁ ਉਧਰੈ ਨਾਨਕ ਹਰਿ ਗੁਨ ਗਾਉ ॥੧॥
tis kai sang sikh uDhrai naanak har gun gaa-o. ||1||
Katika uandamano wa Guru wa Kweli, mwanafunzi anakombolewa kutoka kwa dhambi. Hivyo basi Ee Nanak, unafaa pia kuimba sifa za Mungu katika uandamano wa Guru wa Kweli kama huyo.
ਅਸਟਪਦੀ ॥
asatpadee.
Ashtapadee:
ਸਤਿਗੁਰੁ ਸਿਖ ਕੀ ਕਰੈ ਪ੍ਰਤਿਪਾਲ ॥
satgur sikh kee karai partipaal.
Guru wa Kweli anawathamini wanafunzi wake.
ਸੇਵਕ ਕਉ ਗੁਰੁ ਸਦਾ ਦਇਆਲ ॥
sayvak ka-o gur sadaa da-i-aal.
Guru daima ana huruma kwa mtumishi wake.
ਸਿਖ ਕੀ ਗੁਰੁ ਦੁਰਮਤਿ ਮਲੁ ਹਿਰੈ ॥
sikh kee gur durmat mal hirai.
Guru husafisha uchafu wa fikira najisi akilini mwa mwanafunzi,
ਗੁਰ ਬਚਨੀ ਹਰਿ ਨਾਮੁ ਉਚਰੈ ॥
gur bachnee har naam uchrai.
kwani kwa kufuata ushauri wa Guru, mwanafunzi anakariri Jina la Mungu.
ਸਤਿਗੁਰੁ ਸਿਖ ਕੇ ਬੰਧਨ ਕਾਟੈ ॥
satgur sikh kay banDhan kaatai.
Guru humkomboa mtawa wake kutoka vifungo vya hamu za kidunia.
ਗੁਰ ਕਾ ਸਿਖੁ ਬਿਕਾਰ ਤੇ ਹਾਟੈ ॥
gur kaa sikh bikaar tay haatai.
Msiki (mwanafunzi) wa Guru hujiepusha na vitendo viovu.
ਸਤਿਗੁਰੁ ਸਿਖ ਕਉ ਨਾਮ ਧਨੁ ਦੇਇ ॥
satgur sikh ka-o naam Dhan day-ay.
Guru wa Kweli anampa Siki wake (mwanafunzi) utajiri wa Naam.
ਗੁਰ ਕਾ ਸਿਖੁ ਵਡਭਾਗੀ ਹੇ ॥
gur kaa sikh vadbhaagee hay.
Mwanafunzi wa Guru ana bahati mno.
ਸਤਿਗੁਰੁ ਸਿਖ ਕਾ ਹਲਤੁ ਪਲਤੁ ਸਵਾਰੈ ॥
satgur sikh kaa halat palat savaarai.
Guru wa kweli huimarisha maisha ya mwanafunzi humu na katika dunia itakayofuata.
ਨਾਨਕ ਸਤਿਗੁਰੁ ਸਿਖ ਕਉ ਜੀਅ ਨਾਲਿ ਸਮਾਰੈ ॥੧॥
naanak satgur sikh ka-o jee-a naal samaarai. ||1||
Ee Nanak, Guru wa Kweli humpenda mwanafunzi wake kutoka kwa kiini cha moyo wake.
ਗੁਰ ਕੈ ਗ੍ਰਿਹਿ ਸੇਵਕੁ ਜੋ ਰਹੈ ॥
gur kai garihi sayvak jo rahai.
Mtawa anayeishi kwa mlango ya Guru (daima anatafuta ushauri wa Guru),
ਗੁਰ ਕੀ ਆਗਿਆ ਮਨ ਮਹਿ ਸਹੈ ॥
gur kee aagi-aa man meh sahai.
na hutii Amri za Guru kwa moyo wake wote,
ਆਪਸ ਕਉ ਕਰਿ ਕਛੁ ਨ ਜਨਾਵੈ ॥
aapas ka-o kar kachh na janaavai.
kamwe haonyeshi majivuno kwa njia yoyote,
ਹਰਿ ਹਰਿ ਨਾਮੁ ਰਿਦੈ ਸਦ ਧਿਆਵੈ ॥
har har naam ridai sad Dhi-aavai.
daima anatafakari kuhusu Jina la Mungu,
ਮਨੁ ਬੇਚੈ ਸਤਿਗੁਰ ਕੈ ਪਾਸਿ ॥
man baychai satgur kai paas.
anasalimisha akili yake kwa Guru wa Kweli,
ਤਿਸੁ ਸੇਵਕ ਕੇ ਕਾਰਜ ਰਾਸਿ ॥
tis sayvak kay kaaraj raas.
Shughuli za mtumishi huyo mnyenyekevu zinatatuliwa.
ਸੇਵਾ ਕਰਤ ਹੋਇ ਨਿਹਕਾਮੀ ॥
sayvaa karat ho-ay nihkaamee.
Yule anayetoa huduma isiyo na ubinafsi bila fikira yoyote ya zawadi,
ਤਿਸ ਕਉ ਹੋਤ ਪਰਾਪਤਿ ਸੁਆਮੀ ॥
tis ka-o hot paraapat su-aamee.
Atampata Bwana Mungu wake.