Guru Granth Sahib Translation Project

Guru Granth Sahib Swahili Page 13

Page 13

ਰਾਗੁ ਧਨਾਸਰੀ ਮਹਲਾ ੧ ॥ raag Dhanaasree mehlaa 1. Raag Dhanasari, Guru wa kwanza:
ਗਗਨ ਮੈ ਥਾਲੁ ਰਵਿ ਚੰਦੁ ਦੀਪਕ ਬਨੇ ਤਾਰਿਕਾ ਮੰਡਲ ਜਨਕ ਮੋਤੀ ॥ gagan mai thaal rav chand deepak banay taarikaa mandal janak motee. Ee Mungu, uumbaji wote unatenda Aarti (ibada) yako, anga ni kama sinia ambayo jua na mwezi ni kama taa mbili, na mkusanyiko wa nyota ni kama lulu zilizojaa.
ਧੂਪੁ ਮਲਆਨਲੋ ਪਵਣੁ ਚਵਰੋ ਕਰੇ ਸਗਲ ਬਨਰਾਇ ਫੂਲੰਤ ਜੋਤੀ ॥੧॥ Dhoop mal-aanlo pavan chavro karay sagal banraa-ay foolant jotee. ||1|| Hewa yenye harufu nzuri inayotoka kwenye mlima Malay ni kama ubani, upepo ni kama chavar ya ulimwengu (pepeo) na mimea yote ni kama matoleo ya maua, Ee mwenye Mwangaza.
ਕੈਸੀ ਆਰਤੀ ਹੋਇ ॥ ਭਵ ਖੰਡਨਾ ਤੇਰੀ ਆਰਤੀ ॥ kaisee aartee ho-ay. bhav khandnaa tayree aartee. Ee mwangamizi wa woga (wa kuzaliwa na kufa), ni Aarti (ibada) nzuri yako inayotendwa.
ਅਨਹਤਾ ਸਬਦ ਵਾਜੰਤ ਭੇਰੀ ॥੧॥ ਰਹਾਉ ॥ anhataa sabad vaajant bhayree. ||1|| rahaa-o. Nyimbo takatifu zinazotiririka (sauti ya mipigo ya moyo ya viumbe walio hai) ni kama sauti ya ngoma ikipigwa katika Aartee.
ਸਹਸ ਤਵ ਨੈਨ ਨਨ ਨੈਨ ਹਹਿ ਤੋਹਿ ਕਉ ਸਹਸ ਮੂਰਤਿ ਨਨਾ ਏਕ ਤੋੁਹੀ ॥ sahas tav nain nan nain heh tohi ka-o sahas moorat nanaa ayk tohee. Ee Mungu, una maelfu ya macho (kwa sababu unaenea katika viumbe wote), na ila huna macho (kwa sababu hauna muundo wowote). Una maelfu ya miundo ila hauna muundo wowote wako.
ਸਹਸ ਪਦ ਬਿਮਲ ਨਨ ਏਕ ਪਦ ਗੰਧ ਬਿਨੁ ਸਹਸ ਤਵ ਗੰਧ ਇਵ ਚਲਤ ਮੋਹੀ ॥੨॥ sahas pad bimal nan ayk pad ganDh bin sahas tav ganDh iv chalat mohee. ||2|| Wewe una maelfu ya miguu safi kabisa (kwa sababu unaenea kati ya viumbe wote), ila Wewe huna miguu (kwa sababu huna muundo). Una maelfu ya mapua, ila huna pua. Mchezo huu wako unanistaajabisha.
ਸਭ ਮਹਿ ਜੋਤਿ ਜੋਤਿ ਹੈ ਸੋਇ ॥ sabh meh jot jot hai so-ay. Mwanga au nguvu inayotiririka ndani mwa kila mtu inatokana na Mwanga Mmoja Mkuu (Mungu).
ਤਿਸ ਦੈ ਚਾਨਣਿ ਸਭ ਮਹਿ ਚਾਨਣੁ ਹੋਇ ॥ tis dai chaanan sabh meh chaanan ho-ay. Mwanga (nguvu ya kufikiria) unaoangaza ndani mwa wote, unatokana na Mnara wa Mwanga Mmoja wa milele.
ਗੁਰ ਸਾਖੀ ਜੋਤਿ ਪਰਗਟੁ ਹੋਇ ॥ gur saakhee jot pargat ho-ay. Lakini kuelewa huku kunatambuliwa tu kupitia mafundisho ya Guru (ya kwamba chanzo cha uhai ni sawa katika kila mmoja)
ਜੋ ਤਿਸੁ ਭਾਵੈ ਸੁ ਆਰਤੀ ਹੋਇ ॥੩॥ jo tis bhaavai so aartee ho-ay. ||3|| Hivyo basi, kukubali kinachompendeza Mungu ni ibada yake ya kweli.
ਹਰਿ ਚਰਣ ਕਵਲ ਮਕਰੰਦ ਲੋਭਿਤ ਮਨੋ ਅਨਦਿਨੋੁ ਮੋਹਿ ਆਹੀ ਪਿਆਸਾ ॥ har charan kaval makrand lobhit mano andino mohi aahee pi-aasaa. Ee Mungu, moyo wangu una hamu ya jina lako takatifu, kila siku nina kiu ya nekta ya jina lako.
ਕ੍ਰਿਪਾ ਜਲੁ ਦੇਹਿ ਨਾਨਕ ਸਾਰਿੰਗ ਕਉ ਹੋਇ ਜਾ ਤੇ ਤੇਰੈ ਨਾਇ ਵਾਸਾ ॥੪॥੩॥ kirpaa jal deh naanak saaring ka-o ho-ay jaa tay tayrai naa-ay vaasaa. ||4||3|| Ee Mungu, Nanak anatamani jina lako kama vile ndege wa wimbo anavyotamani tone la mvua, tafadhali tawaza neema yako kwangu ndiposa nibaki nimezama katika jina lako.
ਰਾਗੁ ਗਉੜੀ ਪੂਰਬੀ ਮਹਲਾ ੪ ॥ raag ga-orhee poorbee mehlaa 4. Raag Gauree Poorbee, Guru wa Nne:
ਕਾਮਿ ਕਰੋਧਿ ਨਗਰੁ ਬਹੁ ਭਰਿਆ ਮਿਲਿ ਸਾਧੂ ਖੰਡਲ ਖੰਡਾ ਹੇ ॥ kaam karoDh nagar baho bhari-aa mil saaDhoo khandal khanda hay. Mwili huu wa kibinadamu umejaa maovu ya hasira na usherati, maovu haya yanaweza kuangamizwa tu kwa kukutana na Guru wa kweli.
ਪੂਰਬਿ ਲਿਖਤ ਲਿਖੇ ਗੁਰੁ ਪਾਇਆ ਮਨਿ ਹਰਿ ਲਿਵ ਮੰਡਲ ਮੰਡਾ ਹੇ ॥੧॥ poorab likhat likhay gur paa-i-aa man har liv mandal mandaa hay. ||1|| Lakini ni kwa maandishi yaliyoagizwa mapema tu ambapo Guru anapatikana, ambaye mafundisho yake yanajaa kwenye akili na upendo na kujitolea kwa Mungu.
ਕਰਿ ਸਾਧੂ ਅੰਜੁਲੀ ਪੁਨੁ ਵਡਾ ਹੇ ॥ kar saaDhoo anjulee pun vadaa hay. Fanya ibada kwa Guru kwa unyenyekevu, hili ni tendo la ustahili kuu.
ਕਰਿ ਡੰਡਉਤ ਪੁਨੁ ਵਡਾ ਹੇ ॥੧॥ ਰਹਾਉ ॥ kar dand-ut pun vadaa hay. ||1|| rahaa-o. Sujudu mbele zake; kwa kweli hiki ni kitendo kitakatifu.
ਸਾਕਤ ਹਰਿ ਰਸ ਸਾਦੁ ਨ ਜਾਣਿਆ ਤਿਨ ਅੰਤਰਿ ਹਉਮੈ ਕੰਡਾ ਹੇ ॥ saakat har ras saad na jaani-aa tin antar ha-umai kandaa hay. Wasioamini hawathamini furaha ya kumkumbuka Mungu kwa sababu mwiba wa ubinafsi umepachikwa kwa kina ndani mwao.
ਜਿਉ ਜਿਉ ਚਲਹਿ ਚੁਭੈ ਦੁਖੁ ਪਾਵਹਿ ਜਮਕਾਲੁ ਸਹਹਿ ਸਿਰਿ ਡੰਡਾ ਹੇ ॥੨॥ ji-o ji-o chaleh chubhai dukh paavahi jamkaal saheh sir dandaa hay. ||2|| Wanavyozidi kuishi maisha kwa ubinafsi, wanazidi kuteseka, kana kwamba wanatembea miguu mitupu iliyodungwa na miba. Mwishowe wanapitia mateso ya kifo.
ਹਰਿ ਜਨ ਹਰਿ ਹਰਿ ਨਾਮਿ ਸਮਾਣੇ ਦੁਖੁ ਜਨਮ ਮਰਣ ਭਵ ਖੰਡਾ ਹੇ ॥ har jan har har naam samaanay dukh janam maran bhav khanda hay. (Kwa upande mwingine), watu wanaompenda Mungu wanabaki wamemakinikia kujitolea kwake kwa upendo na wanakombolewa kutoka kwa mzunguko wa kuzaliwa na kufa.
ਅਬਿਨਾਸੀ ਪੁਰਖੁ ਪਾਇਆ ਪਰਮੇਸਰੁ ਬਹੁ ਸੋਭ ਖੰਡ ਬ੍ਰਹਮੰਡਾ ਹੇ ॥੩॥ abhinaasee purakh paa-i-aa parmaysar baho sobh khand barahmanda hay. ||3|| Wanamgundua Mungu Mkuu asiyeangamia, na umaarufu wake unaenea katika maeneo yote ya ulimwengu.
ਹਮ ਗਰੀਬ ਮਸਕੀਨ ਪ੍ਰਭ ਤੇਰੇ ਹਰਿ ਰਾਖੁ ਰਾਖੁ ਵਡ ਵਡਾ ਹੇ ॥ ham gareeb maskeen parabh tayray har raakh raakh vad vadaa hay. Ee Mungu, sisi ni maskini na wapole, lakini sisi ni wako. Wewe ndiwe mkuu kati ya wakuu wote, tafadhali tulinde kutoka kwa maovu haya.
ਜਨ ਨਾਨਕ ਨਾਮੁ ਅਧਾਰੁ ਟੇਕ ਹੈ ਹਰਿ ਨਾਮੇ ਹੀ ਸੁਖੁ ਮੰਡਾ ਹੇ ॥੪॥੪॥ jan naanak naam aDhaar tayk hai har naamay hee sukh mandaa hay. ||4||4|| Ee Nanak, jina la Mungu ni riziki ya pekee na nguzo ya kweli, na ni kupitia kwa Naam tu ambapo tunahisi amani ya mbinguni.
ਰਾਗੁ ਗਉੜੀ ਪੂਰਬੀ ਮਹਲਾ ੫ ॥ raag ga-orhee poorbee mehlaa 5. Raag Gauree Poorbee, na Guru wa Tano:
ਕਰਉ ਬੇਨੰਤੀ ਸੁਣਹੁ ਮੇਰੇ ਮੀਤਾ ਸੰਤ ਟਹਲ ਕੀ ਬੇਲਾ ॥ kara-o baynantee sunhu mayray meetaa sant tahal kee baylaa. Ee rafiki zangu, sikizeni! Nawasilisha kwenu ya kwamba maisha haya ya kibinadamu ni fursa ya kipekee ya kufuata mafundisho ya Guru (kwa sababu ni Guru pekee ambaye anaweza kukubariki kwa Naam).
ਈਹਾ ਖਾਟਿ ਚਲਹੁ ਹਰਿ ਲਾਹਾ ਆਗੈ ਬਸਨੁ ਸੁਹੇਲਾ ॥੧॥ eehaa khaat chalhu har laahaa aagai basan suhaylaa. ||1|| Maisha haya ya kibinadamu ni fursa ya kupata utajiri wa jina la Mungu, ndiposa utakuwa na starehe katika dunia itakayofuata (mahakama ya Mungu).
ਅਉਧ ਘਟੈ ਦਿਨਸੁ ਰੈਣਾਰੇ ॥ a-oDh ghatai dinas rainaaray. Ee akili yangu, kila mchana na usiku maisha ya mtu yanayobaki yanazidi kupungua.
ਮਨ ਗੁਰ ਮਿਲਿ ਕਾਜ ਸਵਾਰੇ ॥੧॥ ਰਹਾਉ ॥ man gur mil kaaj savaaray. ||1|| rahaa-o. Basi tufanikishe maisha haya kwa kufuata mafundisho ya Guru (kabla hatujachelewa).
ਇਹੁ ਸੰਸਾਰੁ ਬਿਕਾਰੁ ਸੰਸੇ ਮਹਿ ਤਰਿਓ ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ॥ ih sansaar bikaar sansay meh tari-o barahm gi-aanee. Dunia hii imezama katika maovu na kutokuaminiana, ni mtu mtakatifu mwenye busara pekee anayeweza kuogelea na kuvuka bahari-dunia ya dhambi.
ਜਿਸਹਿ ਜਗਾਇ ਪੀਆਵੈ ਇਹੁ ਰਸੁ ਅਕਥ ਕਥਾ ਤਿਨਿ ਜਾਨੀ ॥੨॥ jisahi jagaa-ay pee-aavai ih ras akath kathaa tin jaanee. ||2|| Ni yule mmoja pekee, ambaye Mungu anaamsha kutoka usingizi wa ushirika na mambo ya dunia na kuwasaidia kufurahia faraja ya jina lake, anayeelewa siri isiyoweza kuelezwa.
ਜਾ ਕਉ ਆਏ ਸੋਈ ਬਿਹਾਝਹੁ ਹਰਿ ਗੁਰ ਤੇ ਮਨਹਿ ਬਸੇਰਾ ॥ jaa ka-o aa-ay so-ee bihaajhahu har gur tay maneh basayraa. Enyi rafiki zangu, kusanyeni tu utajiri ambao umewaleta duniani humu. Ni kwa kupitia Guru tu ambapo Mungu anaweza kuishi moyoni mwako.
ਨਿਜ ਘਰਿ ਮਹਲੁ ਪਾਵਹੁ ਸੁਖ ਸਹਜੇ ਬਹੁਰਿ ਨ ਹੋਇਗੋ ਫੇਰਾ ॥੩॥ nij ghar mahal paavhu sukh sehjay bahur na ho-igo fayraa. ||3|| Kwa njia hii, utampata Mungu kwa amani na hiari ndani mwako na hakutakuwa tena na mizunguko ya kuzaliwa na kufa kwako.
ਅੰਤਰਜਾਮੀ ਪੁਰਖ ਬਿਧਾਤੇ ਸਰਧਾ ਮਨ ਕੀ ਪੂਰੇ ॥ antarjaamee purakh biDhaatay sarDhaa man kee pooray. Ee Muumba Mkuu unayejua yote, tafadhali timiza hamu hii ya akili yangu.
ਨਾਨਕ ਦਾਸੁ ਇਹੈ ਸੁਖੁ ਮਾਗੈ ਮੋ ਕਉ ਕਰਿ ਸੰਤਨ ਕੀ ਧੂਰੇ ॥੪॥੫॥ naanak daas ihai sukh maagai mo ka-o kar santan kee Dhooray. ||4||5|| Ndiposa nihudumie (nibaki katika kikundi cha) wafuasi wako wa kweli bila ubinafsi, hii ndio furaha pekee anayoulizia mtumishi wako Nanak .


© 2025 SGGS ONLINE
error: Content is protected !!
Scroll to Top