Page 280
ਨਾਨਕ ਸੰਤ ਭਾਵੈ ਤਾ ਓਇ ਭੀ ਗਤਿ ਪਾਹਿ ॥੨॥
naanak sant bhaavai taa o-ay bhee gat paahi. ||2||
Ee Nanak, Mtakatifu apendapo, hata wachongezi wanainuliwa kiroho.
ਸੰਤ ਕਾ ਨਿੰਦਕੁ ਮਹਾ ਅਤਤਾਈ ॥
sant kaa nindak mahaa attaa-ee.
Mchongezi wa Mtakatifu ni mtenda uovu mbaya kabisa.
ਸੰਤ ਕਾ ਨਿੰਦਕੁ ਖਿਨੁ ਟਿਕਨੁ ਨ ਪਾਈ ॥
sant kaa nindak khin tikan na paa-ee.
Mchongezi wa Mtakatifu hapati amani hata kwa muda mfupi.
ਸੰਤ ਕਾ ਨਿੰਦਕੁ ਮਹਾ ਹਤਿਆਰਾ ॥
sant kaa nindak mahaa hati-aaraa.
Mchongezi wa Mtakatifu huwa muuaji katili kabisa.
ਸੰਤ ਕਾ ਨਿੰਦਕੁ ਪਰਮੇਸੁਰਿ ਮਾਰਾ ॥
sant kaa nindak parmaysur maaraa.
Mchongezi wa Mtakatifu hulaaniwa na Mungu.
ਸੰਤ ਕਾ ਨਿੰਦਕੁ ਰਾਜ ਤੇ ਹੀਨੁ ॥
sant kaa nindak raaj tay heen.
Mchongezi wa Mtakatifu hana nguvu ya kidunia na raha.
ਸੰਤ ਕਾ ਨਿੰਦਕੁ ਦੁਖੀਆ ਅਰੁ ਦੀਨੁ ॥
sant kaa nindak dukhee-aa ar deen.
Mchongezi wa Mtakatifu huwa mwenye taabu na maskini.
ਸੰਤ ਕੇ ਨਿੰਦਕ ਕਉ ਸਰਬ ਰੋਗ ॥
sant kay nindak ka-o sarab rog.
Mchongezi wa Mtakatifu anaathiriwa na aina zote za magonjwa.
ਸੰਤ ਕੇ ਨਿੰਦਕ ਕਉ ਸਦਾ ਬਿਜੋਗ ॥
sant kay nindak ka-o sadaa bijog.
Mchongezi wa Mtakatifu milele anatenganishwa kutoka kwa Mungu.
ਸੰਤ ਕੀ ਨਿੰਦਾ ਦੋਖ ਮਹਿ ਦੋਖੁ ॥
sant kee nindaa dokh meh dokh.
Kumchongeza Mtakatifu ni dhambi mbaya zaidi kati ya dhambi zote.
ਨਾਨਕ ਸੰਤ ਭਾਵੈ ਤਾ ਉਸ ਕਾ ਭੀ ਹੋਇ ਮੋਖੁ ॥੩॥
naanak sant bhaavai taa us kaa bhee ho-ay mokh. ||3||
Ee Nanak, ikimpendeza Mtakatifu, hata mchongezi kama huyo atakombolewa.
ਸੰਤ ਕਾ ਦੋਖੀ ਸਦਾ ਅਪਵਿਤੁ ॥
sant kaa dokhee sadaa apvit.
Fikira akilini mwa mchongezi wa Mtakatifu daima zimechafuliwa.
ਸੰਤ ਕਾ ਦੋਖੀ ਕਿਸੈ ਕਾ ਨਹੀ ਮਿਤੁ ॥
sant kaa dokhee kisai kaa nahee mit.
Mchongezi wa Mtakatifu si rafiki wa mtu yeyote.
ਸੰਤ ਕੇ ਦੋਖੀ ਕਉ ਡਾਨੁ ਲਾਗੈ ॥
sant kay dokhee ka-o daan laagai.
Mchongezi wa Mtakatifu huadhibiwa na hakimu wa haki.
ਸੰਤ ਕੇ ਦੋਖੀ ਕਉ ਸਭ ਤਿਆਗੈ ॥
sant kay dokhee ka-o sabh ti-aagai.
Mchongezi wa Mtakatifu huachwa pweke na kila mtu.
ਸੰਤ ਕਾ ਦੋਖੀ ਮਹਾ ਅਹੰਕਾਰੀ ॥
sant kaa dokhee mahaa ahaNkaaree.
Mchongezi wa Mtakatifu amezama katika ubinafsi kabisa.
ਸੰਤ ਕਾ ਦੋਖੀ ਸਦਾ ਬਿਕਾਰੀ ॥
sant kaa dokhee sadaa bikaaree.
Mchongezi wa Mtakatifu daima anajihusisha katika vitendo viovu.
ਸੰਤ ਕਾ ਦੋਖੀ ਜਨਮੈ ਮਰੈ ॥
sant kaa dokhee janmai marai.
Mchongezi wa Mtakatifu huendelea kupitia mizunguko wa kuzaliwa na kufa.
ਸੰਤ ਕੀ ਦੂਖਨਾ ਸੁਖ ਤੇ ਟਰੈ ॥
sant kee dookhnaa sukh tay tarai.
Kwa kumchongeza Mtakatifu, yeye hana amani yoyote.
ਸੰਤ ਕੇ ਦੋਖੀ ਕਉ ਨਾਹੀ ਠਾਉ ॥
sant kay dokhee ka-o naahee thaa-o.
Mchongezi wa Mtakatifu hana pahali pa kujificha.
ਨਾਨਕ ਸੰਤ ਭਾਵੈ ਤਾ ਲਏ ਮਿਲਾਇ ॥੪॥
naanak sant bhaavai taa la-ay milaa-ay. ||4||
Ee Nanak, iwapo inapendeza Mtakatifu, yeye anaunganisha mchongezi kama huyo na Yeye.
ਸੰਤ ਕਾ ਦੋਖੀ ਅਧ ਬੀਚ ਤੇ ਟੂਟੈ ॥
sant kaa dokhee aDh beech tay tootai.
Mchongezi wa Mtakatifu hufeli katikati mwa kufanya kazi yoyote.
ਸੰਤ ਕਾ ਦੋਖੀ ਕਿਤੈ ਕਾਜਿ ਨ ਪਹੂਚੈ ॥
sant kaa dokhee kitai kaaj na pahoochai.
Mchongezi wa Mtakatifu hawezi kutimiza kazi yoyote.
ਸੰਤ ਕੇ ਦੋਖੀ ਕਉ ਉਦਿਆਨ ਭ੍ਰਮਾਈਐ ॥
sant kay dokhee ka-o udi-aan bharmaa-ee-ai.
Mchongezi wa mtakatifu hufanywa kuzurura nyikani.
ਸੰਤ ਕਾ ਦੋਖੀ ਉਝੜਿ ਪਾਈਐ ॥
sant kaa dokhee ujharh paa-ee-ai.
Mchongezi wa Mtakatifu anapotoshwa katika ukiwa.
ਸੰਤ ਕਾ ਦੋਖੀ ਅੰਤਰ ਤੇ ਥੋਥਾ ॥
sant kaa dokhee antar tay thothaa.
Mchongezi wa Mtakatifu hafahamu kusudi halisi la maisha,
ਜਿਉ ਸਾਸ ਬਿਨਾ ਮਿਰਤਕ ਕੀ ਲੋਥਾ ॥
ji-o saas binaa mirtak kee lothaa.
Kama maiti ya mfu, bila pumzi ya uhai.
ਸੰਤ ਕੇ ਦੋਖੀ ਕੀ ਜੜ ਕਿਛੁ ਨਾਹਿ ॥
sant kay dokhee kee jarh kichh naahi.
Mchongezi wa Mtakatifu hana msingi thabiti na wa kiroho.
ਆਪਨ ਬੀਜਿ ਆਪੇ ਹੀ ਖਾਹਿ ॥
aapan beej aapay hee khaahi.
Yeye mwenyewe sharti ale alichopanda. (kuteseka matokeo ya vitendo vyake viovu)
ਸੰਤ ਕੇ ਦੋਖੀ ਕਉ ਅਵਰੁ ਨ ਰਾਖਨਹਾਰੁ ॥
sant kay dokhee ka-o avar na raakhanhaar.
Mchongezi wa Mtakatifu hawezi kukombolewa na yeyote mwengine kutoka kwa tabia hiyo ya kuchongeza.
ਨਾਨਕ ਸੰਤ ਭਾਵੈ ਤਾ ਲਏ ਉਬਾਰਿ ॥੫॥
naanak sant bhaavai taa la-ay ubaar. ||5||
Ee Nanak, iwapo inampendeza Mtakatifu, basi hata mchongezi kama huyo anaokolewa kutoka kwa tabia ya kuchongeza.
ਸੰਤ ਕਾ ਦੋਖੀ ਇਉ ਬਿਲਲਾਇ ॥
sant kaa dokhee i-o billaa-ay.
Mchongezi wa Mtakatifu huomboleza,
ਜਿਉ ਜਲ ਬਿਹੂਨ ਮਛੁਲੀ ਤੜਫੜਾਇ ॥
ji-o jal bihoon machhulee tarhafrhaa-ay.
Kama samaki nje ya maji akikunyata kwa uchungu.
ਸੰਤ ਕਾ ਦੋਖੀ ਭੂਖਾ ਨਹੀ ਰਾਜੈ ॥
sant kaa dokhee bhookhaa nahee raajai.
Mchongezi wa Mtakatifu kamwe hatoshelezwi kutoka kwa hamu ya kuchongeza,
ਜਿਉ ਪਾਵਕੁ ਈਧਨਿ ਨਹੀ ਧ੍ਰਾਪੈ ॥
ji-o paavak eeDhan nahee Dharaapai.
Kama vile moto kamwe hautoshelezwi na kiwango chochote cha kuni.
ਸੰਤ ਕਾ ਦੋਖੀ ਛੁਟੈ ਇਕੇਲਾ ॥
sant kaa dokhee chhutai ikaylaa.
Mchongezi wa Mtakatifu anaachwa peke yake,
ਜਿਉ ਬੂਆੜੁ ਤਿਲੁ ਖੇਤ ਮਾਹਿ ਦੁਹੇਲਾ ॥
ji-o boo-aarh til khayt maahi duhaylaa.
Kama mmea tasa wa ufuta ulioachwa kwenye shamba.
ਸੰਤ ਕਾ ਦੋਖੀ ਧਰਮ ਤੇ ਰਹਤ ॥
sant kaa dokhee Dharam tay rahat.
Mchongezi wa Mtakatifu hana imani yoyote.
ਸੰਤ ਕਾ ਦੋਖੀ ਸਦ ਮਿਥਿਆ ਕਹਤ ॥
sant kaa dokhee sad mithi-aa kahat.
Mchongezi wa Mtakatifu daima husema uongo.
ਕਿਰਤੁ ਨਿੰਦਕ ਕਾ ਧੁਰਿ ਹੀ ਪਇਆ ॥
kirat nindak kaa Dhur hee pa-i-aa.
Mchongezi anafanya kitendo cha kuchongeza kwa sababu ndicho hatima yake iliyoagiziwa mapema.
ਨਾਨਕ ਜੋ ਤਿਸੁ ਭਾਵੈ ਸੋਈ ਥਿਆ ॥੬॥
naanak jo tis bhaavai so-ee thi-aa. ||6||
Ee Nanak, chochote ambacho Mungu anaamuru hicho hutendeka.
ਸੰਤ ਕਾ ਦੋਖੀ ਬਿਗੜ ਰੂਪੁ ਹੋਇ ਜਾਇ ॥
sant kaa dokhee bigarh roop ho-ay jaa-ay.
Mchongezi wa Mtakatifu amefedheheshwa sana, kana kwamba ameharibiwa sura.
ਸੰਤ ਕੇ ਦੋਖੀ ਕਉ ਦਰਗਹ ਮਿਲੈ ਸਜਾਇ ॥
sant kay dokhee ka-o dargeh milai sajaa-ay.
Mchongezi wa Mtakatifu hupokea adhabu katika mahakama ya Mungu.
ਸੰਤ ਕਾ ਦੋਖੀ ਸਦਾ ਸਹਕਾਈਐ ॥
sant kaa dokhee sadaa sahkaa-ee-ai.
Mchongezi wa Mtakatifu daima yu katika uchungu mkali,
ਸੰਤ ਕਾ ਦੋਖੀ ਨ ਮਰੈ ਨ ਜੀਵਾਈਐ ॥
sant kaa dokhee na marai na jeevaa-ee-ai.
Mchongezi wa Mtakatifu ananing’inia kiroho kati ya uhai na kifo.
ਸੰਤ ਕੇ ਦੋਖੀ ਕੀ ਪੁਜੈ ਨ ਆਸਾ ॥
sant kay dokhee kee pujai na aasaa.
Tumaini la mchongezi wa Matakatifu halitimizwi.
ਸੰਤ ਕਾ ਦੋਖੀ ਉਠਿ ਚਲੈ ਨਿਰਾਸਾ ॥
sant kaa dokhee uth chalai niraasaa.
Mchongezi wa Mtakatifu huondoka duniani akiwa ametamauka.
ਸੰਤ ਕੈ ਦੋਖਿ ਨ ਤ੍ਰਿਸਟੈ ਕੋਇ ॥
sant kai dokh na taristai ko-ay.
Kwa kumchongeza Mtakatifu, hakuna mtu anayetoshelezwa kutoka kwa hamu ya kuchongeza.
ਜੈਸਾ ਭਾਵੈ ਤੈਸਾ ਕੋਈ ਹੋਇ ॥
jaisaa bhaavai taisaa ko-ee ho-ay.
Tabia za mtu zinaundwa kulingana na nia zake.
ਪਇਆ ਕਿਰਤੁ ਨ ਮੇਟੈ ਕੋਇ ॥
pa-i-aa kirat na maytai ko-ay.
Vitendo vya awali haviwezi kufutwa na yeyote.
ਨਾਨਕ ਜਾਨੈ ਸਚਾ ਸੋਇ ॥੭॥
naanak jaanai sachaa so-ay. ||7||
Ee Nanak, ni Mungu wa milele pekee anayejua fumbo hili.
ਸਭ ਘਟ ਤਿਸ ਕੇ ਓਹੁ ਕਰਨੈਹਾਰੁ ॥
sabh ghat tis kay oh karnaihaar.
Viumbe vyote ni miliki yake, na Yeye ndiye Muumba.
ਸਦਾ ਸਦਾ ਤਿਸ ਕਉ ਨਮਸਕਾਰੁ ॥
sadaa sadaa tis ka-o namaskaar.
Daima na milele, sujudu kwake kwa heshima.
ਪ੍ਰਭ ਕੀ ਉਸਤਤਿ ਕਰਹੁ ਦਿਨੁ ਰਾਤਿ ॥
parabh kee ustat karahu din raat.
Imba sifa za Mungu, mchana na usiku.
ਤਿਸਹਿ ਧਿਆਵਹੁ ਸਾਸਿ ਗਿਰਾਸਿ ॥
tiseh Dhi-aavahu saas giraas.
Tafakari kumhusu Yeye kila wakati
ਸਭੁ ਕਛੁ ਵਰਤੈ ਤਿਸ ਕਾ ਕੀਆ ॥
sabh kachh vartai tis kaa kee-aa.
Kila kitu hutendeka kulingana na kutenda kwake.
ਜੈਸਾ ਕਰੇ ਤੈਸਾ ਕੋ ਥੀਆ ॥
jaisaa karay taisaa ko thee-aa.
Vile ambavyo Mungu anamtengeneza mtu, ndivyo binadamu huwa.
ਅਪਨਾ ਖੇਲੁ ਆਪਿ ਕਰਨੈਹਾਰੁ ॥
apnaa khayl aap karnaihaar.
Yeye Mwenyewe ndiye mtekelezaji wa mchezo wake.
ਦੂਸਰ ਕਉਨੁ ਕਹੈ ਬੀਚਾਰੁ ॥
doosar ka-un kahai beechaar.
Nani mwengine anayeweza kusema au kujadili kuhusu haya?