Guru Granth Sahib Translation Project

Guru Granth Sahib Swahili Page 922

Page 922

ਕਹੈ ਨਾਨਕੁ ਪ੍ਰਭੁ ਆਪਿ ਮਿਲਿਆ ਕਰਣ ਕਾਰਣ ਜੋਗੋ ॥੩੪॥ kahai naanak parabh aap mili-aa karan kaaran jogo. ||34|| Nanak anasema, Mungu Mwenyewe, awezaye kufanya chochote, amekutana nami.
ਏ ਸਰੀਰਾ ਮੇਰਿਆ ਇਸੁ ਜਗ ਮਹਿ ਆਇ ਕੈ ਕਿਆ ਤੁਧੁ ਕਰਮ ਕਮਾਇਆ ॥ ay sareeraa mayri-aa is jag meh aa-ay kai ki-aa tuDh karam kamaa-i-aa. Ee mwili wangu, umetenda vitendo vipi vya maana kwa kuja duniani?
ਕਿ ਕਰਮ ਕਮਾਇਆ ਤੁਧੁ ਸਰੀਰਾ ਜਾ ਤੂ ਜਗ ਮਹਿ ਆਇਆ ॥ ke karam kamaa-i-aa tuDh sareeraa jaa too jag meh aa-i-aa. Naam, Ee mwili wangu, tangu ulipokuja duniani, umetenda vitendo vipi vizuri?
ਜਿਨਿ ਹਰਿ ਤੇਰਾ ਰਚਨੁ ਰਚਿਆ ਸੋ ਹਰਿ ਮਨਿ ਨ ਵਸਾਇਆ ॥ jin har tayraa rachan rachi-aa so har man na vasaa-i-aa. Wewe hujatathmini akilini mwako Mungu huyo aliyekuumba.
ਗੁਰ ਪਰਸਾਦੀ ਹਰਿ ਮੰਨਿ ਵਸਿਆ ਪੂਰਬਿ ਲਿਖਿਆ ਪਾਇਆ ॥ gur parsaadee har man vasi-aa poorab likhi-aa paa-i-aa. Kwa Neema ya Guru, Mungu anaishi akilini mwa mtu ambaye hatima yake ilipangwa mapema imetimizwa.
ਕਹੈ ਨਾਨਕੁ ਏਹੁ ਸਰੀਰੁ ਪਰਵਾਣੁ ਹੋਆ ਜਿਨਿ ਸਤਿਗੁਰ ਸਿਉ ਚਿਤੁ ਲਾਇਆ ॥੩੫॥ kahai naanak ayhu sareer parvaan ho-aa jin satgur si-o chit laa-i-aa. ||35|| Nanak anasema, yeye akaziaye akili yake kwa mafundisho ya Guru, ametimiza kusudi la maisha ya kibinadamu na ameidhinishwa mbele ya Mungu.
ਏ ਨੇਤ੍ਰਹੁ ਮੇਰਿਹੋ ਹਰਿ ਤੁਮ ਮਹਿ ਜੋਤਿ ਧਰੀ ਹਰਿ ਬਿਨੁ ਅਵਰੁ ਨ ਦੇਖਹੁ ਕੋਈ ॥ ay naytarahu mayriho har tum meh jot Dharee har bin avar na daykhhu ko-ee. Ee macho yangu, Mungu ameweka Mwanga Wake ndani mwako; hivyo basi usitazame mwingine ila Mungu (haswa uone Mungu akienea katika kila mmoja na kila mahali).
ਹਰਿ ਬਿਨੁ ਅਵਰੁ ਨ ਦੇਖਹੁ ਕੋਈ ਨਦਰੀ ਹਰਿ ਨਿਹਾਲਿਆ ॥ har bin avar na daykhhu ko-ee nadree har nihaali-aa. Usione kitu kingine isipokuwa Mungu akienea kote, Mungu pekee ndiye astahili kutazamwa
ਏਹੁ ਵਿਸੁ ਸੰਸਾਰੁ ਤੁਮ ਦੇਖਦੇ ਏਹੁ ਹਰਿ ਕਾ ਰੂਪੁ ਹੈ ਹਰਿ ਰੂਪੁ ਨਦਰੀ ਆਇਆ ॥ ayhu vis sansaar tum daykh-day ayhu har kaa roop hai har roop nadree aa-i-aa. Ee macho yangu, dunia hii nzima unayoitazama ni udhihirisho wa Mungu; ni muundo huu wa Mungu, ambao macho yangu yanaona.
ਗੁਰ ਪਰਸਾਦੀ ਬੁਝਿਆ ਜਾ ਵੇਖਾ ਹਰਿ ਇਕੁ ਹੈ ਹਰਿ ਬਿਨੁ ਅਵਰੁ ਨ ਕੋਈ ॥ gur parsaadee bujhi-aa jaa vaykhaa har ik hai har bin avar na ko-ee. Kwa Neema ya Guru, nimegundua hili, na sasa popote ninapoangalia, naona tu Mungu Mmoja, na pasipo Mungu hakuna yeyote mwengine.
ਕਹੈ ਨਾਨਕੁ ਏਹਿ ਨੇਤ੍ਰ ਅੰਧ ਸੇ ਸਤਿਗੁਰਿ ਮਿਲਿਐ ਦਿਬ ਦ੍ਰਿਸਟਿ ਹੋਈ ॥੩੬॥ kahai naanak ayhi naytar anDh say satgur mili-ai dib darisat ho-ee. ||36|| Nanak anasema: Hapo awali macho haya yalikuwa kipofu kiroho, nilipokutana na Guru wa kweli, mwanga mtakatifu ulikuja ndani mwao na sasa macho haya yanaona Mungu kila mahali.
ਏ ਸ੍ਰਵਣਹੁ ਮੇਰਿਹੋ ਸਾਚੈ ਸੁਨਣੈ ਨੋ ਪਠਾਏ ॥ ay sarvanhu mayriho saachai sunnai no pathaa-ay. Ee masikio yangu, umetumwa humu kusikiliza sifa za Mungu tu.
ਸਾਚੈ ਸੁਨਣੈ ਨੋ ਪਠਾਏ ਸਰੀਰਿ ਲਾਏ ਸੁਣਹੁ ਸਤਿ ਬਾਣੀ ॥ saachai sunnai no pathaa-ay sareer laa-ay sunhu sat banee. Naam, umeambatishwa kwa mwili na kutumwa humu kusikiliza maneno matakatifu ya Guru ya sifa za Mungu.
ਜਿਤੁ ਸੁਣੀ ਮਨੁ ਤਨੁ ਹਰਿਆ ਹੋਆ ਰਸਨਾ ਰਸਿ ਸਮਾਣੀ ॥ jit sunee man tan hari-aa ho-aa rasnaa ras samaanee. Akili na mwili zinasisimka kwa kusikiliza maneno takatifu ya Guru ya sifa za Mungu na ulimi unazamishwa katika nekta ya Naam.
ਸਚੁ ਅਲਖ ਵਿਡਾਣੀ ਤਾ ਕੀ ਗਤਿ ਕਹੀ ਨ ਜਾਏ ॥ sach alakh vidaanee taa kee gat kahee na jaa-ay. Mungu ni wa ajabu mno na hawezi kufahamika, hali Yake haiwezi kuelezwa.
ਕਹੈ ਨਾਨਕੁ ਅੰਮ੍ਰਿਤ ਨਾਮੁ ਸੁਣਹੁ ਪਵਿਤ੍ਰ ਹੋਵਹੁ ਸਾਚੈ ਸੁਨਣੈ ਨੋ ਪਠਾਏ ॥੩੭॥ kahai nanak amrit naam sunhu pavitar hovhu saachai sunnai no pathaaay. ||37|| Nanak anasema, sikiliza Naam ya ambrosia na uwe mtakatifu, uliumbwa kusikiliza Neno takatifu tu.
ਹਰਿ ਜੀਉ ਗੁਫਾ ਅੰਦਰਿ ਰਖਿ ਕੈ ਵਾਜਾ ਪਵਣੁ ਵਜਾਇਆ ॥ har jee-o gufaa andar rakh kai vaajaa pavan vajaa-i-aa. Kwa kuweka roho kwa mwili kama pango, Mungu alipuliza pumzi ya uhai ndani mwake kama ipuliziwavyo hewa kwa ala ya muziki.
ਵਜਾਇਆ ਵਾਜਾ ਪਉਣ ਨਉ ਦੁਆਰੇ ਪਰਗਟੁ ਕੀਏ ਦਸਵਾ ਗੁਪਤੁ ਰਖਾਇਆ ॥ vajaa-i-aa vaajaa pa-un na-o du-aaray pargat kee-ay dasvaa gupat rakhaa-i-aa. Naam, Mungu alipuliza pumzi ya uhai ndani ya mwili na kudhihirisha viungo tisa vya mwili kwa milango tisa (macho mawili, masikio mawili, mianzi miwili ya pua, ulimi mmoja, na njia mbili za mkojo na kinyesi) lakini aliuficha mlango wa kumi.
ਗੁਰਦੁਆਰੈ ਲਾਇ ਭਾਵਨੀ ਇਕਨਾ ਦਸਵਾ ਦੁਆਰੁ ਦਿਖਾਇਆ ॥ gurdu-aarai laa-ay bhaavnee iknaa dasvaa du-aar dikhaa-i-aa. I Kwa yule ambaye Mungu alibariki na upendo kwa Naam kupitia kwa Guru, Yeye alimdhihirishia mlango wa kumi pia.
ਤਹ ਅਨੇਕ ਰੂਪ ਨਾਉ ਨਵ ਨਿਧਿ ਤਿਸ ਦਾ ਅੰਤੁ ਨ ਜਾਈ ਪਾਇਆ ॥ tah anayk roop naa-o nav niDh tis daa ant na jaa-ee paa-i-aa. Katika hali hiyo kuu ya kiroho ambapo mlango wa kumi umedhihirishwa, mtu anagundua utajiri usio na kikomo wa Jina la Mungu katika miundo mingi mizuri.
ਕਹੈ ਨਾਨਕੁ ਹਰਿ ਪਿਆਰੈ ਜੀਉ ਗੁਫਾ ਅੰਦਰਿ ਰਖਿ ਕੈ ਵਾਜਾ ਪਵਣੁ ਵਜਾਇਆ ॥੩੮॥ kahai nanak har piaarai jeeo gufaa andar rakh kai vajaa pavan vajaaiaa. ||38|| Nanak anasema, kwa kuweka roho katika mwili kama pango, Mungu mpendwa alipuliza pumzi ya uhai ndani mwake kama ipulizwavyo hewa katika ala ya muziki.
ਏਹੁ ਸਾਚਾ ਸੋਹਿਲਾ ਸਾਚੈ ਘਰਿ ਗਾਵਹੁ ॥ ayhu sachaa sohila saachai ghar gaavhu. Imba wimbo huu halisi wa sifa za Mungu katika ushirika mtakatifu
ਗਾਵਹੁ ਤ ਸੋਹਿਲਾ ਘਰਿ ਸਾਚੈ ਜਿਥੈ ਸਦਾ ਸਚੁ ਧਿਆਵਹੇ ॥ gaavhu ta sohila ghar saachai jithai sadaa sach Dhi-aavhay. Ndio, imba wimbo huu wa raha tele katika ushirika mtakatifu, ambapo daima wanatafakari kwa upendo kuhusu Mungu wa milele.
ਸਚੋ ਧਿਆਵਹਿ ਜਾ ਤੁਧੁ ਭਾਵਹਿ ਗੁਰਮੁਖਿ ਜਿਨਾ ਬੁਝਾਵਹੇ ॥ sacho Dhi-aavahi jaa tuDh bhaaveh gurmukh jinaa bujhaavhay. Ee Mungu, wanakutafakari Wewe wakati unaokupendeza tu, na kwa yule ambaye Wewe unabariki na uelewa huu kwa njia ya Guru.
ਇਹੁ ਸਚੁ ਸਭਨਾ ਕਾ ਖਸਮੁ ਹੈ ਜਿਸੁ ਬਖਸੇ ਸੋ ਜਨੁ ਪਾਵਹੇ ॥ ih sach sabhnaa kaa khasam hai jis bakhsay so jan paavhay. Mungu wa milele ni Bwana wa wote, wanaomgundua Yeye ni ambao Yeye anakuwa mwenye neema kwao.
ਕਹੈ ਨਾਨਕੁ ਸਚੁ ਸੋਹਿਲਾ ਸਚੈ ਘਰਿ ਗਾਵਹੇ ॥੩੯॥ kahai naanak sach sohilaa sachai ghar gaavhay. ||39|| Nanak anasema, kwa kujiunga na ushirika mtakatifu, wanaimba sifa za Mungu.
ਅਨਦੁ ਸੁਣਹੁ ਵਡਭਾਗੀਹੋ ਸਗਲ ਮਨੋਰਥ ਪੂਰੇ ॥ anad sunhu vadbhaageeho sagal manorath pooray. Enyi wenye bahati nzuri, sikilizeni wimbo wa raha tele; kwa kusikiliza wimbo huu, matakwa yenu yote yatatimizwa.
ਪਾਰਬ੍ਰਹਮੁ ਪ੍ਰਭੁ ਪਾਇਆ ਉਤਰੇ ਸਗਲ ਵਿਸੂਰੇ ॥ paarbarahm parabh paa-i-aa utray sagal visooray. Wale ambao wameusikiliza wimbo wa raha tele wamemgundua Mungu, na mahangaiko yao yote yameondolewa
ਦੂਖ ਰੋਗ ਸੰਤਾਪ ਉਤਰੇ ਸੁਣੀ ਸਚੀ ਬਾਣੀ ॥ dookh rog santaap utray sunee sachee banee. Kwa kusikiliza Neno Takatifu, huzuni na taabu zao zote zimeondoka.
ਸੰਤ ਸਾਜਨ ਭਏ ਸਰਸੇ ਪੂਰੇ ਗੁਰ ਤੇ ਜਾਣੀ ॥ sant saajan bha-ay sarsay pooray gur tay jaanee. Kwa kuelewa neno takatifu kutoka kwa Guru wa kweli, watakatifu na marafiki wote wanafurahia.
ਸੁਣਤੇ ਪੁਨੀਤ ਕਹਤੇ ਪਵਿਤੁ ਸਤਿਗੁਰੁ ਰਹਿਆ ਭਰਪੂਰੇ ॥ suntay puneet kahtay pavit satgur rahi-aa bharpooray. Wale wanaosikiliza au kutamka neno la Guru, huwa watakatifu wanapomwona Guru wa kweli kwa wimbo huu, wimbo wa raha tele.
ਬਿਨਵੰਤਿ ਨਾਨਕੁ ਗੁਰ ਚਰਣ ਲਾਗੇ ਵਾਜੇ ਅਨਹਦ ਤੂਰੇ ॥੪੦॥੧॥ binvant naanak gur charan laagay vaajay anhad tooray. ||40||1|| Nanak anawasilisha kwa unyenyekevu kwamba wale wanaomakinikia neno la Guru, raha tele hujaa ndani yao kana kwamba melodia takatifu zisizo na mwisho zinacheza akilini mwao.


© 2025 SGGS ONLINE
error: Content is protected !!
Scroll to Top