Page 294
ਬਨਿ ਤਿਨਿ ਪਰਬਤਿ ਹੈ ਪਾਰਬ੍ਰਹਮੁ ॥
ban tin parbat hai paarbarahm.
Mungu Mkuu anapenyeza katika nyika, nyanjani na milimani.
ਜੈਸੀ ਆਗਿਆ ਤੈਸਾ ਕਰਮੁ ॥
jaisee aagi-aa taisaa karam.
Kama ilivyo amri yake, ndivyo kilivyo kitendo cha kiumbe.
ਪਉਣ ਪਾਣੀ ਬੈਸੰਤਰ ਮਾਹਿ ॥
pa-un paanee baisantar maahi.
Yeye anapenyeza upepo, maji na moto.
ਚਾਰਿ ਕੁੰਟ ਦਹ ਦਿਸੇ ਸਮਾਹਿ ॥
chaar kunt dah disay samaahi.
Yeye anaenea katika pembe zote nne na katika mielekeo yote kumi (yupo kila mahali).
ਤਿਸ ਤੇ ਭਿੰਨ ਨਹੀ ਕੋ ਠਾਉ ॥
tis tay bhinn nahee ko thaa-o.
Hakuna mahali ambapo hayupo Yeye.
ਗੁਰ ਪ੍ਰਸਾਦਿ ਨਾਨਕ ਸੁਖੁ ਪਾਉ ॥੨॥
gur parsaad naanak sukh paa-o. ||2||
Ee Nanak, amani inapokelewa kwa Neema ya Guru.
ਬੇਦ ਪੁਰਾਨ ਸਿੰਮ੍ਰਿਤਿ ਮਹਿ ਦੇਖੁ ॥
bayd puraan simrit meh daykh.
Mtazame Yeye katika mafundisho ya Vedas, Puranas na Smritis.
ਸਸੀਅਰ ਸੂਰ ਨਖ੍ਯ੍ਯਤ੍ਰ ਮਹਿ ਏਕੁ ॥
sasee-ar soor nakh-yatar meh ayk.
Yuyo huyo Mmoja anapenyeza katika mwezi, jua na nyota.
ਬਾਣੀ ਪ੍ਰਭ ਕੀ ਸਭੁ ਕੋ ਬੋਲੈ ॥
banee prabh kee sabh ko bolai.
Kila mtu anatamka neno la Mungu,
ਆਪਿ ਅਡੋਲੁ ਨ ਕਬਹੂ ਡੋਲੈ ॥
aap adol na kabhoo dolai.
Lakini licha ya kuwepo katika vyote, Yeye Mwenyewe hatikisiki na kamwe hayumbi.
ਸਰਬ ਕਲਾ ਕਰਿ ਖੇਲੈ ਖੇਲ ॥
sarab kalaa kar khaylai khayl.
Baada ya kuumba nguvu zote, Yeye anacheza michezo ya kidunia.
ਮੋਲਿ ਨ ਪਾਈਐ ਗੁਣਹ ਅਮੋਲ ॥
mol na paa-ee-ai gunah amol.
Fadhila zake haziwezi kukadiriwa na utukufu wake hauwezi kuchunguzwa.
ਸਰਬ ਜੋਤਿ ਮਹਿ ਜਾ ਕੀ ਜੋਤਿ ॥
sarab jot meh jaa kee jot.
yeye, ambaye mwanga wake unaangazia viumbe vyote,
ਧਾਰਿ ਰਹਿਓ ਸੁਆਮੀ ਓਤਿ ਪੋਤਿ ॥
Dhaar rahi-o su-aamee ot pot.
Bwana huyo anatoa msaada kwa wote tena na tena.
ਗੁਰ ਪਰਸਾਦਿ ਭਰਮ ਕਾ ਨਾਸੁ ॥
gur parsaad bharam kaa naas.
Wale, ambao shaka yao inaondolewa kwa neema ya Guru.
ਨਾਨਕ ਤਿਨ ਮਹਿ ਏਹੁ ਬਿਸਾਸੁ ॥੩॥
naanak tin meh ayhu bisaas. ||3||
Ee Nanak, wana imani imara kwamba Mungu ana uwezo wote.
ਸੰਤ ਜਨਾ ਕਾ ਪੇਖਨੁ ਸਭੁ ਬ੍ਰਹਮ ॥
sant janaa kaa paykhan sabh barahm.
Watakatifu humwona Mungu kila mahali.
ਸੰਤ ਜਨਾ ਕੈ ਹਿਰਦੈ ਸਭਿ ਧਰਮ ॥
sant janaa kai hirdai sabh Dharam.
Katika moyo wa Watakatifu, fikira zote zinazotokea ni za uadilifu.
ਸੰਤ ਜਨਾ ਸੁਨਹਿ ਸੁਭ ਬਚਨ ॥
sant janaa suneh subh bachan.
Watakatifu husikiliza maneno ya fadhili pekee,
ਸਰਬ ਬਿਆਪੀ ਰਾਮ ਸੰਗਿ ਰਚਨ ॥
sarab bi-aapee raam sang rachan.
Na daima wanabaki wamezama katika Mungu anayeenea kote.
ਜਿਨਿ ਜਾਤਾ ਤਿਸ ਕੀ ਇਹ ਰਹਤ ॥
jin jaataa tis kee ih rahat.
Ndivyo ulivyo mtindo wa maisha wa yule ambaye amemgundua Mungu
ਸਤਿ ਬਚਨ ਸਾਧੂ ਸਭਿ ਕਹਤ ॥
sat bachan saaDhoo sabh kahat.
Mtakatifu huyo hutamka maneno matakatifu pekee (maneno ya sifa za Mungu).
ਜੋ ਜੋ ਹੋਇ ਸੋਈ ਸੁਖੁ ਮਾਨੈ ॥
jo jo ho-ay so-ee sukh maanai.
Chochote kinachotendeka, anakubali kwa amani.
ਕਰਨ ਕਰਾਵਨਹਾਰੁ ਪ੍ਰਭੁ ਜਾਨੈ ॥
karan karaavanhaar parabh jaanai.
Yeye anamfahamu, Mungu kama Mtendaji, Msingi wa misingi yote.
ਅੰਤਰਿ ਬਸੇ ਬਾਹਰਿ ਭੀ ਓਹੀ ॥
antar basay baahar bhee ohee.
Anaamini kwamba Mungu huyo mmoja anayeishi ndani mwake pia yupo nje.
ਨਾਨਕ ਦਰਸਨੁ ਦੇਖਿ ਸਭ ਮੋਹੀ ॥੪॥
naanak darsan daykh sabh mohee. ||4||
Ee Nanak, kwa kuutazama muonekano huu wa Mungu unaoenea kote, dunia nzima inavutiwa.
ਆਪਿ ਸਤਿ ਕੀਆ ਸਭੁ ਸਤਿ ॥
aap sat kee-aa sabh sat.
Yeye Mwenyewe ni wa Kweli, na vyote alivyoviumba ni vya Kweli wala si njozi.
ਤਿਸੁ ਪ੍ਰਭ ਤੇ ਸਗਲੀ ਉਤਪਤਿ ॥
tis parabh tay saglee utpat.
Uumbaji mzima umetokana na Mungu.
ਤਿਸੁ ਭਾਵੈ ਤਾ ਕਰੇ ਬਿਸਥਾਰੁ ॥
tis bhaavai taa karay bisthaar.
Inavyompendeza Yeye, anauumba upanuzi huu,
ਤਿਸੁ ਭਾਵੈ ਤਾ ਏਕੰਕਾਰੁ ॥
tis bhaavai taa aikankaar.
Na inavyompendeza, Yeye anakuwa Mmoja na tena wa kipekee.
ਅਨਿਕ ਕਲਾ ਲਖੀ ਨਹ ਜਾਇ ॥
anik kalaa lakhee nah jaa-ay.
Nyingi ni nguvu zake ambazo haziwezi kujulikana.
ਜਿਸੁ ਭਾਵੈ ਤਿਸੁ ਲਏ ਮਿਲਾਇ ॥
jis bhaavai tis la-ay milaa-ay.
Yeye humuunganisha yeyote anayetaka naye mwenyewe.
ਕਵਨ ਨਿਕਟਿ ਕਵਨ ਕਹੀਐ ਦੂਰਿ ॥
kavan nikat kavan kahee-ai door.
Haiwezi kusemwa nani yu karibu na Yeye na nani yu mbali naye,
ਆਪੇ ਆਪਿ ਆਪ ਭਰਪੂਰਿ ॥
aapay aap aap bharpoor.
Kwa sababu Yeye Mwenyewe anaenea kote.
ਅੰਤਰਗਤਿ ਜਿਸੁ ਆਪਿ ਜਨਾਏ ॥
antargat jis aap janaa-ay.
Kwa yule anayempa uelewa huu wa hali ya juu ya kiroho,
ਨਾਨਕ ਤਿਸੁ ਜਨ ਆਪਿ ਬੁਝਾਏ ॥੫॥
naanak tis jan aap bujhaa-ay. ||5||
Ee Nanak, kwa mtu huyo Yeye anajidhihirisha.
ਸਰਬ ਭੂਤ ਆਪਿ ਵਰਤਾਰਾ ॥
sarab bhoot aap vartaaraa.
Yeye Mwenyewe anaenea katika viumbe vyote,
ਸਰਬ ਨੈਨ ਆਪਿ ਪੇਖਨਹਾਰਾ ॥
sarab nain aap paykhanhaaraa.
Kupitia kwa macho yote, Yeye Mwenyewe ndiye anayetazama.
ਸਗਲ ਸਮਗ੍ਰੀ ਜਾ ਕਾ ਤਨਾ ॥
sagal samagree jaa kaa tanaa.
Uumbaji wote ni Mwili wake.
ਆਪਨ ਜਸੁ ਆਪ ਹੀ ਸੁਨਾ ॥
aapan jas aap hee sunaa.
Yeye Mwenyewe huisikiliza Sifa yake Mwenyewe.
ਆਵਨ ਜਾਨੁ ਇਕੁ ਖੇਲੁ ਬਨਾਇਆ ॥
aavan jaan ik khayl banaa-i-aa.
Mungu ameumba sarakasi ya kuzaliwa na kufa.
ਆਗਿਆਕਾਰੀ ਕੀਨੀ ਮਾਇਆ ॥
aagi-aakaaree keenee maa-i-aa.
Na kuifanya Maya itii Mapenzi yake.
ਸਭ ਕੈ ਮਧਿ ਅਲਿਪਤੋ ਰਹੈ ॥
sabh kai maDh alipato rahai.
Kati ya hayo yote, Yeye anabaki amejitenga.
ਜੋ ਕਿਛੁ ਕਹਣਾ ਸੁ ਆਪੇ ਕਹੈ ॥
jo kichh kahnaa so aapay kahai.
Chochote kinachopaswa kusemwa, Yeye Mwenyewe husema.
ਆਗਿਆ ਆਵੈ ਆਗਿਆ ਜਾਇ ॥
aagi-aa aavai aagi-aa jaa-ay.
Kwa amri yake, mtu huzaliwa na kwa amri yake, mtu hufa.
ਨਾਨਕ ਜਾ ਭਾਵੈ ਤਾ ਲਏ ਸਮਾਇ ॥੬॥
naanak jaa bhaavai taa la-ay samaa-ay. ||6||
Ee Nanak, inapompendeza, Yeye anawaunganisha ndani yake.
ਇਸ ਤੇ ਹੋਇ ਸੁ ਨਾਹੀ ਬੁਰਾ ॥
is tay ho-ay so naahee buraa.
Chochote kinachotoka kwake hakiwezi kuwa kibaya.
ਓਰੈ ਕਹਹੁ ਕਿਨੈ ਕਛੁ ਕਰਾ ॥
orai kahhu kinai kachh karaa.
Isipokuwa Yeye, nani anayeweza kufanya chochote?
ਆਪਿ ਭਲਾ ਕਰਤੂਤਿ ਅਤਿ ਨੀਕੀ ॥
aap bhalaa kartoot at neekee.
Yeye Mwenyewe ni mzuri; matendo yake ni mazuri zaidi.
ਆਪੇ ਜਾਨੈ ਅਪਨੇ ਜੀ ਕੀ ॥
aapay jaanai apnay jee kee.
Yeye peke yake anajua kilicho akilini mwake.
ਆਪਿ ਸਾਚੁ ਧਾਰੀ ਸਭ ਸਾਚੁ ॥
aap saach Dhaaree sabh saach.
Yeye ni wa Kweli, na vyote ambavyo ameanzilisha pia ni vya Kweli wala si njozi.
ਓਤਿ ਪੋਤਿ ਆਪਨ ਸੰਗਿ ਰਾਚੁ ॥
ot pot aapan sang raach.
Yeye amechanganyikana na uumbaji wake, kabisa kabisa.
ਤਾ ਕੀ ਗਤਿ ਮਿਤਿ ਕਹੀ ਨ ਜਾਇ ॥
taa kee gat mit kahee na jaa-ay.
Ukuu na kadiri yake haiwezi kuelezwa.
ਦੂਸਰ ਹੋਇ ਤ ਸੋਝੀ ਪਾਇ ॥
doosar ho-ay ta sojhee paa-ay.
Iwapo kungekuwa na mwengine kama Yeye, wakati huo tu ndipo mtu anagemuelewa Yeye.
ਤਿਸ ਕਾ ਕੀਆ ਸਭੁ ਪਰਵਾਨੁ ॥
tis kaa kee-aa sabh parvaan.
Kila kitu kinachofanywa na Yeye lazima kikubalike na wote.
ਗੁਰ ਪ੍ਰਸਾਦਿ ਨਾਨਕ ਇਹੁ ਜਾਨੁ ॥੭॥
gur parsaad naanak ih jaan. ||7||
Ee Nanak, hili linajulikana tu kupitia neema ya Guru.
ਜੋ ਜਾਨੈ ਤਿਸੁ ਸਦਾ ਸੁਖੁ ਹੋਇ ॥
jo jaanai tis sadaa sukh ho-ay.
Yule anayemgundua Yeye, hupokea amani ya kudumu milele.
ਆਪਿ ਮਿਲਾਇ ਲਏ ਪ੍ਰਭੁ ਸੋਇ ॥
aap milaa-ay la-ay parabh so-ay.
Mungu humuunganisha mtu huyo naye Mwenyewe.
ਓਹੁ ਧਨਵੰਤੁ ਕੁਲਵੰਤੁ ਪਤਿਵੰਤੁ ॥
oh Dhanvant kulvant pativant.
Mtu huyo ni tajiri wa kiroho, wa familia bora na mwenye heshima,
ਜੀਵਨ ਮੁਕਤਿ ਜਿਸੁ ਰਿਦੈ ਭਗਵੰਤੁ ॥
jeevan mukat jis ridai bhagvant.
Yule ambaye Mungu anaishi moyoni mwake anakuwa huru kutoka kwa mzunguko wa kuzaliwa na kufa akiwa bado hai.
ਧੰਨੁ ਧੰਨੁ ਧੰਨੁ ਜਨੁ ਆਇਆ ॥
Dhan Dhan Dhan jan aa-i-aa.
Umebarikiwa kabisa ujio wa binadamu kama huyo duniani,