Guru Granth Sahib Translation Project

Guru Granth Sahib Swahili Page 273

Page 273

ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਕੀ ਦ੍ਰਿਸਟਿ ਅੰਮ੍ਰਿਤੁ ਬਰਸੀ ॥ barahm gi-aanee kee darisat amrit barsee. Nekta ya ambrosia inamiminwa kutoka kwa mtazamo wa mtu anayemfahamu Mungu.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਬੰਧਨ ਤੇ ਮੁਕਤਾ ॥ barahm gi-aanee banDhan tay muktaa. Mtu anayemfahamu Mungu yuko huru kutoka kwa misongamano ya kidunia.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਕੀ ਨਿਰਮਲ ਜੁਗਤਾ ॥ barahm gi-aanee kee nirmal jugtaa. Mtindo wa maisha wa mtu mwenye hekima takatifu ni safi bila doa na huru kutoka kwa maovu.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਕਾ ਭੋਜਨੁ ਗਿਆਨ ॥ barahm gi-aanee kaa bhojan gi-aan. Hekima ya kiroho ni lishe ya mtu anayemfahamu Mungu.
ਨਾਨਕ ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਕਾ ਬ੍ਰਹਮ ਧਿਆਨੁ ॥੩॥ naanak barahm gi-aanee kaa barahm Dhi-aan. ||3|| Ee Nanak, mtu anayemfahamu Mungu amezama katika utafakari wa Mungu.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਏਕ ਊਪਰਿ ਆਸ ॥ barahm gi-aanee ayk oopar aas. Mtu anayemfahamu Mungu anaweka matumaini yake kwa yule Mmoja pekee.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਕਾ ਨਹੀ ਬਿਨਾਸ ॥ barahm gi-aanee kaa nahee binaas. Hali ya juu ya kiroho ya mtu anayemfahamu Mungu kamwe haiharibiki.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਕੈ ਗਰੀਬੀ ਸਮਾਹਾ ॥ barahm gi-aanee kai gareebee samaahaa. Mtu anayemfahamu Mungu amejawa na unyenyekevu.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਪਰਉਪਕਾਰ ਉਮਾਹਾ ॥ barahm gi-aanee par-upkaar omaahaa. Mtu anayemfahamu Mungu daima anafurahia kuwatendea wengine mema.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਕੈ ਨਾਹੀ ਧੰਧਾ ॥ barahm gi-aanee kai naahee DhanDhaa. Mtu anayemfahamu Mungu hana misongamano ya kidunia.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਲੇ ਧਾਵਤੁ ਬੰਧਾ ॥ barahm gi-aanee lay Dhaavat banDhaa. Mtu anayemfahamu Mungu anaidhibiti akili yake inayozurura.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਕੈ ਹੋਇ ਸੁ ਭਲਾ ॥ barahm gi-aanee kai ho-ay so bhalaa. Kwa mtu anayemfahamu Mungu chochote kinachotendeka ni kwa wema.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਸੁਫਲ ਫਲਾ ॥ barahm gi-aanee sufal falaa. Kwa njia hii, mtu anayemfahamu Mungu anafanikiwa na kusitawi katika kila hali ya maisha.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਸੰਗਿ ਸਗਲ ਉਧਾਰੁ ॥ barahm gi-aanee sang sagal uDhaar. Katika Uandamano wa mtu anayemfahamu Mungu, wote wanakombolewa kutoka kwa dhambi.
ਨਾਨਕ ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਜਪੈ ਸਗਲ ਸੰਸਾਰੁ ॥੪॥ naanak barahm gi-aanee japai sagal sansaar. ||4|| Ee Nanak, kupitia mtu anayemfahamu Mungu, dunia nzima inatafakari kumhusu Mungu.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਕੈ ਏਕੈ ਰੰਗ ॥ barahm gi-aanee kai aikai rang. Mtu anayemfahamu Mungu daima amejawa na upendo kwa Mungu.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਕੈ ਬਸੈ ਪ੍ਰਭੁ ਸੰਗ ॥ barahm gi-aanee kai basai parabh sang. Mungu daima anaishi katika uandamano wa mtu anayemfahamu.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਕੈ ਨਾਮੁ ਆਧਾਰੁ ॥ barahm gi-aanee kai naam aaDhaar. Jina la Mungu ndilo riziki ya mtu anayemfahamu.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਕੈ ਨਾਮੁ ਪਰਵਾਰੁ ॥ barahm gi-aanee kai naam parvaar. Kwa mtu anayemfahamu Mungu Naam ni familia yake.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਸਦਾ ਸਦ ਜਾਗਤ ॥ barahm gi-aanee sadaa sad jaagat. Mtu anayemfahamu Mungu anabaki kutahadhari dhidi ya athari za maovu.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਅਹੰਬੁਧਿ ਤਿਆਗਤ ॥ barahm gi-aanee ahaN-buDh ti-aagat. Mtu anayemfahamu Mungu hukana fikira zake za ubinafsi.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਕੈ ਮਨਿ ਪਰਮਾਨੰਦ ॥ barahm gi-aanee kai man parmaanand. Mungu, chanzo cha raha tele kuu, anaishi akilini mwa mtu anayemfahamu.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਕੈ ਘਰਿ ਸਦਾ ਅਨੰਦ ॥ barahm gi-aanee kai ghar sadaa anand. Kuna raha tele inayodumu milele moyoni mwa mtu anayemfahamu Mungu.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਸੁਖ ਸਹਜ ਨਿਵਾਸ ॥ barahm gi-aanee sukh sahj nivaas. Mtu anayemfahamu Mungu huishi kwa amani na utulivu wa hisia na silika.
ਨਾਨਕ ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਕਾ ਨਹੀ ਬਿਨਾਸ ॥੫॥ naanak barahm gi-aanee kaa nahee binaas. ||5|| Ee Nanak, hali kuu ya kiroho ya mtu anayemfahamu Mungu kamwe haiharibiki.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਬ੍ਰਹਮ ਕਾ ਬੇਤਾ ॥ barahm gi-aanee barahm kaa baytaa. Mtu anayemfahamu Mungu anamjua Mungu.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਏਕ ਸੰਗਿ ਹੇਤਾ ॥ barahm gi-aanee ayk sang haytaa. Mtu anayemfahamu Mungu anapenda yule Mmoja pekee.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਕੈ ਹੋਇ ਅਚਿੰਤ ॥ barahm gi-aanee kai ho-ay achint. Mtu anayemfahamu Mungu yuko huru kutoka kwa wasiwasi wowote.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਕਾ ਨਿਰਮਲ ਮੰਤ ॥ barahm gi-aanee kaa nirmal mant. Safi ni mafundisho ya mtu anayemfahamu Mungu.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਜਿਸੁ ਕਰੈ ਪ੍ਰਭੁ ਆਪਿ ॥ barahm gi-aanee jis karai parabh aap. Mtu anayemfahamu Mungu anafanywa awe hivyo na Mungu Mwenyewe.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਕਾ ਬਡ ਪਰਤਾਪ ॥ barahm gi-aanee kaa bad partaap. Mkuu ni utukufu wa mtu anayemfahamu Mungu.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਕਾ ਦਰਸੁ ਬਡਭਾਗੀ ਪਾਈਐ ॥ barahm gi-aanee kaa daras badbhaagee paa-ee-ai. Kwa bahati nzuri mtu anabarikiwa na maono ya mtu anayemfahamu Mungu.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਕਉ ਬਲਿ ਬਲਿ ਜਾਈਐ ॥ barahm gi-aanee ka-o bal bal jaa-ee-ai. Hebu tujitie wakfu kwa mtu anayemfahamu Mungu.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਕਉ ਖੋਜਹਿ ਮਹੇਸੁਰ ॥ barahm gi-aanee ka-o khojeh mahaysur. Hata miungu kama Bwana Shiva wanatafuta mtu anayemfahamu Mungu.
ਨਾਨਕ ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਆਪਿ ਪਰਮੇਸੁਰ ॥੬॥ naanak barahm gi-aanee aap parmaysur. ||6|| Ee Nanak, mtu anayemfahamu Mungu ni udhihirisho wa Mungu Mwenyewe.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਕੀ ਕੀਮਤਿ ਨਾਹਿ ॥ barahm gi-aanee kee keemat naahi. Fadhila za mtu anayemfahamu Mungu haziwezi kukadirika.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਕੈ ਸਗਲ ਮਨ ਮਾਹਿ ॥ barahm gi-aanee kai sagal man maahi. Fadhila zote, hudumu katika mtu anayemfahamu Mungu.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਕਾ ਕਉਨ ਜਾਨੈ ਭੇਦੁ ॥ barahm gi-aanee kaa ka-un jaanai bhayd. Nani anayeweza kujua fumbo la maisha mema ya mtu anayemfahamu Mungu?
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਕਉ ਸਦਾ ਅਦੇਸੁ ॥ barahm gi-aanee ka-o sadaa adays. Daima sujudu kwa heshima kwa mtu anayemfahamu Mungu.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਕਾ ਕਥਿਆ ਨ ਜਾਇ ਅਧਾਖ੍ਯ੍ਯਰੁ ॥ barahm gi-aanee kaa kathi-aa na jaa-ay aDhaakh-yar. Hata chembe cha utukufu wa mtu anayemfahamu Mungu hakiwezi kuelezwa.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਸਰਬ ਕਾ ਠਾਕੁਰੁ ॥ barahm gi-aanee sarab kaa thaakur. mtu anayemfahamu Mungu anaenziwa na wote.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਕੀ ਮਿਤਿ ਕਉਨੁ ਬਖਾਨੈ ॥ barahm gi-aanee kee mit ka-un bakhaanai. Nani anayeweza kueleza kadiri ya fadhila za mtu anayemfahamu Mungu?
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਕੀ ਗਤਿ ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਜਾਨੈ ॥ barahm gi-aanee kee gat barahm gi-aanee jaanai. Ni Mtu anayemfahamu Mungu pekee anayejua hali ya juu ya akili ya kumfahamu Mungu.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਕਾ ਅੰਤੁ ਨ ਪਾਰੁ ॥ barahm gi-aanee kaa ant na paar. Fadhila za mtu anayemfahamu Mungu hazina kikomo.
ਨਾਨਕ ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਕਉ ਸਦਾ ਨਮਸਕਾਰੁ ॥੭॥ naanak barahm gi-aanee ka-o sadaa namaskaar. ||7|| Ee Nanak, sujudu kwa heshima kwa mtu anayemfahamu Mungu.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਸਭ ਸ੍ਰਿਸਟਿ ਕਾ ਕਰਤਾ ॥ barahm gi-aanee sabh sarisat kaa kartaa. Mtu anayemfahamu Mungu ndiye Muumba wa uumbaji wote.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਸਦ ਜੀਵੈ ਨਹੀ ਮਰਤਾ ॥ barahm gi-aanee sad jeevai nahee martaa. Mtu anayemfahamu Mungu huishi milele, wala hafi.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਮੁਕਤਿ ਜੁਗਤਿ ਜੀਅ ਕਾ ਦਾਤਾ ॥ barahm gi-aanee mukat jugat jee-a kaa daataa. Mtu anayemfahamu Mungu ndiye mtawaza wa njia ya kufanikisha hali kuu ya kiroho na ukombozi wa roho.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਪੂਰਨ ਪੁਰਖੁ ਬਿਧਾਤਾ ॥ barahm gi-aanee pooran purakh biDhaataa. Mtu anayemfahamu Mungu ndiye Kiumbe Mkuu Kamili, anayepanga mambo yote.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਅਨਾਥ ਕਾ ਨਾਥੁ ॥ barahm gi-aanee anaath kaa naath. Mtu anayemfahamu Mungu ndiye mlinzi wa wasio na ulinzi.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਕਾ ਸਭ ਊਪਰਿ ਹਾਥੁ ॥ barahm gi-aanee kaa sabh oopar haath. Mtu anayemfahamu Mungu hunyoosha mkono wake wa msaada kwa wote.
ਬ੍ਰਹਮ ਗਿਆਨੀ ਕਾ ਸਗਲ ਅਕਾਰੁ ॥ barahm gi-aanee kaa sagal akaar. Ulimwengu mzima ni miliki ya mtu anayemfahamu Mungu.


© 2025 SGGS ONLINE
error: Content is protected !!
Scroll to Top