Guru Granth Sahib Translation Project

Guru Granth Sahib Swahili Page 10

Page 10

ਜਿਨਿ ਦਿਨੁ ਕਰਿ ਕੈ ਕੀਤੀ ਰਾਤਿ ॥ jin din kar kai keetee raat. Yule Mmoja aliyeumba mchana na usiku.
ਖਸਮੁ ਵਿਸਾਰਹਿ ਤੇ ਕਮਜਾਤਿ ॥ khasam visaareh tay kamjaat. Wale wanaomsahau Bwana (Mungu) kama huyo ni wabaya na wa kudharauliwa.
ਨਾਨਕ ਨਾਵੈ ਬਾਝੁ ਸਨਾਤਿ ॥੪॥੩॥ naanak naavai baajh sanaat. ||4||3|| Ee Nanak, mtu asiye na Naam (ukumbuko wa Mungu) ni aibu.
ਰਾਗੁ ਗੂਜਰੀ ਮਹਲਾ ੪ ॥ raag goojree mehlaa 4. Raag Gujari, na Guru wa Nnne:
ਹਰਿ ਕੇ ਜਨ ਸਤਿਗੁਰ ਸਤ ਪੁਰਖਾ ਹਉ ਬਿਨਉ ਕਰਉ ਗੁਰ ਪਾਸਿ ॥ har kay jan satgur sat purkhaa ha-o bin-o kara-o gur paas. Ee binadamu wa Mungu, Guru wa kweli, roho iliyoinuliwa, natoa sala yangu nyenyekevu kwako
ਹਮ ਕੀਰੇ ਕਿਰਮ ਸਤਿਗੁਰ ਸਰਣਾਈ ਕਰਿ ਦਇਆ ਨਾਮੁ ਪਰਗਾਸਿ ॥੧॥ ham keeray kiram satgur sarnaa-ee kar da-i-aa naam pargaas. ||1|| ya kwamba mimi ni mtu duni na mnyenyekevu ambaye amekuja kwenye kimbilio lako, tafadhali nionee huruma na uniangazie kwa jina la Mungu.
ਮੇਰੇ ਮੀਤ ਗੁਰਦੇਵ ਮੋ ਕਉ ਰਾਮ ਨਾਮੁ ਪਰਗਾਸਿ ॥ mayray meet gurdayv mo ka-o raam naam pargaas. Ee rafiki wangu wa dhati, Guru mtakatifu, tafadhali niangazie kwa jina la Mungu.
ਗੁਰਮਤਿ ਨਾਮੁ ਮੇਰਾ ਪ੍ਰਾਨ ਸਖਾਈ ਹਰਿ ਕੀਰਤਿ ਹਮਰੀ ਰਹਰਾਸਿ ॥੧॥ ਰਹਾਉ ॥ gurmat naam mayraa paraan sakhaa-ee har keerat hamree rahraas. ||1|| rahaa-o. Kupitia mafundisho ya Guru, naomba jina la Mungu liwe mkombozi wangu (mwenza wa maisha) na kuimba sifa zake kuwe utajiri wangu wa kweli.
ਹਰਿ ਜਨ ਕੇ ਵਡਭਾਗ ਵਡੇਰੇ ਜਿਨ ਹਰਿ ਹਰਿ ਸਰਧਾ ਹਰਿ ਪਿਆਸ ॥ har jan kay vadbhaag vadayray jin har har sarDhaa har pi-aas. Wamebahatika sana wanaompenda Mungu ambao daima wanajitolea kwa upendo na kuwa na hamu ya Mungu.
ਹਰਿ ਹਰਿ ਨਾਮੁ ਮਿਲੈ ਤ੍ਰਿਪਤਾਸਹਿ ਮਿਲਿ ਸੰਗਤਿ ਗੁਣ ਪਰਗਾਸਿ ॥੨॥ har har naam milai tariptaasahi mil sangat gun pargaas. ||2|| Wanapobarikiwa na jina lake, wanatoshelezwa (hawaathiriwi na Maya). Katika kikundi cha watu wanaompenda Mungu, wanaangaziwa na fadhila.
ਜਿਨ੍ਹ੍ ਹਰਿ ਹਰਿ ਹਰਿ ਰਸੁ ਨਾਮੁ ਨ ਪਾਇਆ ਤੇ ਭਾਗਹੀਣ ਜਮ ਪਾਸਿ ॥ jinH har har har ras naam na paa-i-aa tay bhaagheen jam paas. (Kwa upande mwingine) wale ambao hawajapata kionjo cha jina lake takatifu, hawana bahati kabisa, daima wanabaki na uwoga wa kifo.
ਜੋ ਸਤਿਗੁਰ ਸਰਣਿ ਸੰਗਤਿ ਨਹੀ ਆਏ ਧ੍ਰਿਗੁ ਜੀਵੇ ਧ੍ਰਿਗੁ ਜੀਵਾਸਿ ॥੩॥ jo satgur saran sangat nahee aa-ay Dharig jeevay Dharig jeevaas. ||3|| Wale ambao hawajaja kwenye makao ya Guru wa kweli wala hawatafuti kikundi cha watu wanaompenda Mungu, ni aibu kama viumbe vinavyoishi, uhai wao ni aibu.
ਜਿਨ ਹਰਿ ਜਨ ਸਤਿਗੁਰ ਸੰਗਤਿ ਪਾਈ ਤਿਨ ਧੁਰਿ ਮਸਤਕਿ ਲਿਖਿਆ ਲਿਖਾਸਿ ॥ jin har jan satgur sangat paa-ee tin Dhur mastak likhi-aa likhaas. Wale watu wanaompenda Mungu ambao walikuwa na bahati nzuri ya kuwepo katika kikundi cha Guru wa kweli, walikuwa waliopangiwa tokea mwanzo (kupata Guru wa kweli).
ਧੰਨੁ ਧੰਨੁ ਸਤਸੰਗਤਿ ਜਿਤੁ ਹਰਿ ਰਸੁ ਪਾਇਆ ਮਿਲਿ ਜਨ ਨਾਨਕ ਨਾਮੁ ਪਰਗਾਸਿ ॥੪॥੧॥ Dhan Dhan satsangat jit har ras paa-i-aa mil naanak naam pargaas. ||4||1|| Ee Nanak, umebarikiwa ushirika huo mtakatifu, ambako wanafurahia kionjo cha furaha tele cha jina lake. Ni ushirika wa roho zilizobahatika kama hizo unaoangazia akili na jina lake takatifu.
ਰਾਗੁ ਗੂਜਰੀ ਮਹਲਾ ੫ ॥ raag goojree mehlaa 5. Raag Gujari, na Guru wa tano:
ਕਾਹੇ ਰੇ ਮਨ ਚਿਤਵਹਿ ਉਦਮੁ ਜਾ ਆਹਰਿ ਹਰਿ ਜੀਉ ਪਰਿਆ ॥ kaahay ray man chitvahi udam jaa aahar har jee-o pari-aa. Ee akili yangu, kwa nini unaendelea kuwa na wasiwasi kuhusu lishe yako, wakati Mungu mwenyewe anashughulika?
ਸੈਲ ਪਥਰ ਮਹਿ ਜੰਤ ਉਪਾਏ ਤਾ ਕਾ ਰਿਜਕੁ ਆਗੈ ਕਰਿ ਧਰਿਆ ॥੧॥ sail pathar meh jant upaa-ay taa kaa rijak aagai kar Dhari-aa. ||1|| Hata kwa viumbe alioumba kwenye mawe na miamba, alitoa lishe yao mbeleni.
ਮੇਰੇ ਮਾਧਉ ਜੀ ਸਤਸੰਗਤਿ ਮਿਲੇ ਸੁ ਤਰਿਆ ॥ mayray maaDha-o jee satsangat milay se tari-aa. Ee Bwana wangu mtakatifu, watu wanaoishi katika kikundi cha wafuasi wako wanaokolewa kutoka kwa wasiwasi kama huo.
ਗੁਰ ਪਰਸਾਦਿ ਪਰਮ ਪਦੁ ਪਾਇਆ ਸੂਕੇ ਕਾਸਟ ਹਰਿਆ ॥੧॥ ਰਹਾਉ ॥ gur parsaad param pad paa-i-aa sookay kaasat hari-aa. ||1|| rahaa-o. Kwa neema ya Guru wale wanaofikia hadhi kuu (kutoshelezwa kwa imani kamili kwa Mungu) wanakuwa hai kiroho kama vile mti uliokauka huwa kijani kibichi unapomwagiwa maji.
ਜਨਨਿ ਪਿਤਾ ਲੋਕ ਸੁਤ ਬਨਿਤਾ ਕੋਇ ਨ ਕਿਸ ਕੀ ਧਰਿਆ ॥ janan pitaa lok sut banitaa ko-ay na kis kee Dhari-aa. Wazazi, marafiki, watoto na wenzi wa ndoa – hakuna anayemsaidia mwingine.
ਸਿਰਿ ਸਿਰਿ ਰਿਜਕੁ ਸੰਬਾਹੇ ਠਾਕੁਰੁ ਕਾਹੇ ਮਨ ਭਉ ਕਰਿਆ ॥੨॥ sir sir rijak sambaahay thaakur kaahay man bha-o kari-aa. ||2|| Ee akili yangu, Mungu anatoa riziki ya kila mmoja. Kwa nini una woga sana kuhusu hilo?
ਊਡੈ ਊਡਿ ਆਵੈ ਸੈ ਕੋਸਾ ਤਿਸੁ ਪਾਛੈ ਬਚਰੇ ਛਰਿਆ ॥ oodai ood aavai sai kosaa tis paachhai bachray chhari-aa. Flamingo wanapepea mamia ya maili, wakiwacha wana wao nyuma.
ਤਿਨ ਕਵਨੁ ਖਲਾਵੈ ਕਵਨੁ ਚੁਗਾਵੈ ਮਨ ਮਹਿ ਸਿਮਰਨੁ ਕਰਿਆ ॥੩॥ un kavan khalaavai kavan chugaavai man meh simran kari-aa. ||3|| Nani huwalisha hao vifaranga wadogo? Nani huwafunza kujilisha? (hakuna mtu wa kuwalisha). Mama flamingo daima huwakumbuka vifaranga wake (na ukumbuko huu wenyewe unawaweka hai).
ਸਭ ਨਿਧਾਨ ਦਸ ਅਸਟ ਸਿਧਾਨ ਠਾਕੁਰ ਕਰ ਤਲ ਧਰਿਆ ॥ sabh niDhaan das asat sidhaan thaakur kar tal Dhari-aa. Ee Mungu, inaonekana ya kwamba hazina zote na nguvu za miujiza zisizo za kawaida, unaweza kuzifikia kwa urahisi.
ਜਨ ਨਾਨਕ ਬਲਿ ਬਲਿ ਸਦ ਬਲਿ ਜਾਈਐ ਤੇਰਾ ਅੰਤੁ ਨ ਪਾਰਾਵਰਿਆ ॥੪॥੧॥ jan naanak bal bal sad bal jaa-ee-ai tayraa ant na paraavari-aa. ||4||1|| Ee Nanak, jiweke wakfu kwa Bwana mzuri kama huyo na useme: Ee Mungu, hakuna mwisho wa uumbaji wako, Wewe hauna vikomo.
ਆਸਾ ਮਹਲਾ ੪ ਸੋ ਪੁਰਖੁ raag aasaa mehlaa 4 so purakh Raag Aasaa, na Guru wa nne, So Purakh:
ੴ ਸਤਿਗੁਰ ਪ੍ਰਸਾਦਿ ॥ ik-oNkaar satgur parsaad. Muumba Mmoja Mkuu wa pekee, anayegunduliwa kwa neema ya Guru wa kweli:
ਸੋ ਪੁਰਖੁ ਨਿਰੰਜਨੁ ਹਰਿ ਪੁਰਖੁ ਨਿਰੰਜਨੁ ਹਰਿ ਅਗਮਾ ਅਗਮ ਅਪਾਰਾ ॥ so purakh niranjan har purakh niranjan har agmaa agam apaaraa. Mungu huyo safi kabisa (huru kutoka ushawishi wa viambatanisho vya kidunia), hawezi kueleweka,hafikiiki wala hana vikomo vyovyote.
ਸਭਿ ਧਿਆਵਹਿ ਸਭਿ ਧਿਆਵਹਿ ਤੁਧੁ ਜੀ ਹਰਿ ਸਚੇ ਸਿਰਜਣਹਾਰਾ ॥ sabh Dhi-aavahi sabh Dhi-aavahi tuDh jee har sachay sirjanhaaraa. Ee Muumba wa kweli, kila mtu anatafakari kukuhusu kwa kujitolea kwa upendo.
ਸਭਿ ਜੀਅ ਤੁਮਾਰੇ ਜੀ ਤੂੰ ਜੀਆ ਕਾ ਦਾਤਾਰਾ ॥ sabh jee-a tumaaray jee tooN jee-aa kaa daataaraa. Ee Mungu, viumbe wanaoishi ni wako na wewe ndiye mtoa huduma kwao.
ਹਰਿ ਧਿਆਵਹੁ ਸੰਤਹੁ ਜੀ ਸਭਿ ਦੂਖ ਵਿਸਾਰਣਹਾਰਾ ॥ har Dhi-aavahu santahu jee sabh dookh visaaranhaaraa. Enyi watakatifu wangu wapendwa, tafakarini kuhusu Mungu kwa upendo na kujitolea, ambaye ni mwangamizi wa huzuni yote.
ਹਰਿ ਆਪੇ ਠਾਕੁਰੁ ਹਰਿ ਆਪੇ ਸੇਵਕੁ ਜੀ ਕਿਆ ਨਾਨਕ ਜੰਤ ਵਿਚਾਰਾ ॥੧॥ har aapay thaakur har aapay sayvak jee ki-aa naanak jant vichaaraa. ||1|| Ee Nanak, Mungu mwenyewe ndiye Bwana na Yeye mwenyewe ndiye mtumishi Viumbe wataishije (bila Yeye)?


© 2025 SGGS ONLINE
error: Content is protected !!
Scroll to Top